Na Khalfan Said, Dar es Salaam
NAIBU
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, pichani anayeongea amelitaka Shirika la Umeme
Tanzania TANESCO kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanakamilisha mradi wa
ujenzi wa kituo cha kupoza na kusamabaza umeme kinachotarajiwa kujengwa huko
Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Kalemani ametoa maelekezo hayo leo Agosti 22, 2017, wakati alipofanya ziara
kukagua miradi ya umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini, Kigamboni na
eneo panapotarajiwa kujengwa kituo kingine cha kupoza na kusambaza umeme huko
Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Hakikisheni
mradi wa uejenzi wa kituo hiki cha Kimbiji unakamilika ifikapo Machi 30, mwakani,(2018), na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni,
chukueni mafundi waliokamilisha kazi ya kujenga kituo cha umeme kule Mtwara
waje hapa, muwaache wale wanaojenga transition (njia ya kusafirisha umeme) wajenge, lakini wale mafundi
wengine waleteni hapa ili mradi huu ukamilike.” Alifafanua.
Akiwa
kwenye kituo cha kupoza na kusamabza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam,
Dkt. Kalemani aliipongeza TANESCO kwa juhudi kubwa walizofanya kwa hatua ujenzi waliyofikia ambapo sasa wameanza kufunga mashine kubwa. Kituo
cha Kurasini ndicho kinachotegemewa sana na watu wa Mbagala, Kurasini na Kigamboni.
Ongezeko
la haraka la wakazi kwenye maeneo ya Mbagala, na Kigamboni kumepelekea uhitaji
mkubwa wa umeme ambapo umeme unaopatikana kwa sasa umekuwa haukidhi mahitaji ya
wakazi wa maeneo hayo.
“Naomba
niwaambie, mradi huu umechelewa sana, hivyo basi ongezeni kasi ili ifikapo Agosti 30, mwaka huu,
mradi ukamilike nataka watu wa Mbagala, watu wa Kurasini, na watu wa Kigamboni
wanaondokana na kero hii ya umeme, na mimi nitawaambia washeshimiwa wabunge wa
Kigamboni Mheshimiwa Ndungulile (Dkt. Faustin Ndungulile) na Mheshimiwa
Mangungu (Murtaza Magungu) Mbunge wa Mbagala kuhusu habari hii ili wawaambie
wananchi wa maeneo haya wawe wavumilivu kwani mradi huu sasa utakamilika.”
Alisema.
Dkt.
Kalemani pia aliwaagiza viongozi wa TANESCO, kuhakikisha wanakusanya nguvu kwa
maana ya vifaa kutoka ofisi zote za TANESCO mkoa wa Dar es Salaam, ili
kuhakikisha wananchi wote wa Kigamboni wanaofikia 350 waliolipia ada za kuunganishiwa umeme
wawe wamepelekewe umeme ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Agosti.Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka,
aliwaambia waandishi wa habari kuwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu waziri
yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuhakikisha kero hiyo inaondoka.
Msaidizi
wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid
James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt.
Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo
cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam
Dkt. Kalemani (katikati), akitoa maagizo kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wa Kurasini. |
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), akiwa na Msaidizi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid
James, (kushoto), akiongea na waandishi wa habari.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa
Temeke, Mhandisi Jahulula akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo ambalo patajengwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani
Meneja wa TANESCO Mkoa
wa
Temeke, Mhandisi Jahulula, (wapili kulia), akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo ambalo
patajengwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji, Kigamboni
jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Dkt. Medard Kalemani(katikati).
Fundi wa TANESCO akiwa kazini pale Kigamboni
Mhandisi Jahulula, (kushoto), akionyesha mahala mpaka wa eneo hilo la mradi unapoishia.
No comments:
Post a Comment