MKAZI wa Dodoma nchini Tanzania, Innocent Nyalia, ameibuka na
ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue
Nguvu ya Buku’, katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.
Droo hiyo ilichezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, ambaye kwa
pamoja alishuhudia kupatikana kwa mshindi huyo wa droo ya 29 ya Biko.
Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Masoko na
Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alimpongeza mshindi huyo wa mjini Dodoma,
Nyalia na kuwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa za mamilioni ya Biko.
Alisema huu ni wakati wa kutajirika kwa kuvuna mamilioni ya
Biko yanayoendelea kutolewa kwa wingi, ikiwa ni mwendelezo wa kuona wachezaji
hao wanaotumia simu za M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa kwa kuingiza namba ya
kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 wananeemeka na Biko.
“Kama kawaida yetu ushindi wa Biko ni rahisi kupatikana na
kucheza kwake kuliko michezo mingine yoyote, hivyo tunawaomba Watanzania
wasilaze damu katika mchezo wetu wa Biko unaozidi kutoa mamilioni ya fedha.
“Mbali na ushindi mkubwa wa Sh Milioni 20 unaopatikana
Jumapili na Jumatano, pia zipo zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000,
10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa moja
kwa moja kwa kupitia simu zao walizotumia kuchezea,” Alisema Melles.
Naye Ngolo, mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, aliendelea kuwakumbusha Watanzania jinsi ya kutumia muda wao kwa
kucheza mchezo wa Biko ili wajipatie maendeleo makubwa kutoka Biko.
“Wakati Bodi yetu ikiwapongeza washindi wote wanaoshinda
zawadi kubwa na ndogo kutoka Biko, pia nitumie muda huu kuwataka kila mmoja
kuona fursa ya michezo ya kubahatisha hususan wa Biko ambao unachezwa kwa
kufuata taratibu zote za nchi yetu,” Alisema.
Kwa kutangazwa kwake mshindi, sasa mkazi huyo wa Dodoma
anatarajiwa kukukabidhiwa mamilioni yake mapema wiki hii ili aziweke katika
matumizi yake ya kawaida katika hali ya kukuza uchumi wake, ikiwa ni siku
chache baada ya mshindi wa droo ya 28, Moses Matagili, mkazi wa Goba, kupokea
fedha zake wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment