Katika picha ni viongozi wa Madaktari wakiwa na
Balozi Hemedi Mgaza na Afisa wa Ubalozi Bw. Ahmada Sufiani walipofika
Ubalozi mjini Riyadh kujitambulisha.
Na Mwandishi Maalumu,
Riyadh- Saudi Arabia
Kundi la madaktari
bingwa 18 wa hiyari kutoka nchini Saudi Arabia linatarajiwa kuwasili tarehe 12
Oktoba ambapo wataweka kambi ya tiba (medical camp) kwa muda wa majuma miwili. Madaktari
hao wanatarajiwa kufanya matibabu na upasuaji katika hospitali za kisiwa cha
Pemba.
Akizungumza katika
Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh wakati wa hafla ya kuagana na
madaktari hao, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, alisema
kambi tiba hii ni ya pili kufanyika Zanzibar. Mwezi Novemba mwaka 2016
madaktari hao walifika Zanzibar na kuweka kambi ya kwanza katika kisiwa cha
Pemba kwa mara ya kwanza kwa mafanikio makubwa.
Mwaka jana madaktari hao
walipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya ya
Zanzibar na madaktari wenyeji, ndio maana wamependelea kurejea tena mwaka huu.
Pamoja na kutoa
huduma za matibabu, madaktari hao watakwenda na dawa na vifaa tiba vya aina
mbalimbali ambavyo Mwisho wa kambi watavitoa kama msaada kwenye hospitali hizo.
No comments:
Post a Comment