Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia
mwenye fulana ya Biko akimkabidhi fedha zake mshindi wao wa Bahati
Nasibu, Mohamed Kivugo aliyeibuka kidedea katika droo ya 33
iliyochezeshwa Jumapili. Kushoto ni Afisa wa NMB, Tawi la Bank House,
Posta jijini Dar es Salaam akishuhudia makabidhiano hayo.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
FUNDI
magari mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Mohamed Kivugo mwenye
miaka 45, amesema kwamba fedha zake alizokabidhiwa jana baada ya kushinda
kwenye Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', atazitumia kujengea
nyumba ili aondokane na changamoto ya makazi.
Kivugo
aliyasema hayo jana wakati anapokea zawadi ya Sh Milioni 20 za ushindi wa
Biko alizokabidhiwa katika benki ya NMB, tawi la Bank House Posta,
jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko, Mohamed Kivugo akiwa ameshika fedha zake baada ya kukabidhiwa jana katika Tawi la NMB la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam tayari kwa matumizi yake ya kawaida.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo, Kivugo alisema dhamira yake kubwa ni kutatua
changamoto ya makazi kwa kuzitumia fedha za Biko kujenga nyumba.
"Ingawa
nimepata ushauri mzuri kutoka kwa watu wa NMB baada ya kukabidhiwa
fedha zangu kutoka Biko baada ya kushinda kwenye droo ya 33
iliyochezeshwa Jumapili, lakini naamini wazo la nyumba ni zuri kwangu.
"Nawashauri
Watanzania wenzangu wacheze Biko mara nyingi na wasikate tamaa ili
waweze kuibuka na ushindi kama nilivyoibuka mimi, ukizingatia kuwa biko
ni bahati nasibu inayotoa ushindi na kukabidhi fedha kwa Jataka,
"Alisema.
Naye Mratibu wa
Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, aliwataka Watanzania
kucheza Biko ili wavune utajiri mkubwa kutoka kwenye bahati nasibu yao
inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala
kuanzia Sh 1000 na kuendelea katika Tigo Pesa, MPesa na Airtel Money
huku namba ya Kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.
"Kushinda
Biko ni rahisi pamoja na kupokea zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000,
10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh milioni moja zinazolipwa
moja kwa moja kwenye simu za washindi wanazotumia kuchezea Biko bila
kusahau donge nono la Sh Milioni 20 inayotoka kila Jumatano na Jumapili
kama aliyoshinda mshindi wetu Kivugo wa Tabata," Alisema.
Kwa
mujibu wa Melles, zaidi ya Sh Bilioni mbili zimelipwa kwa washindi
katika miezi mitatu ya Mei, Juni na Julai, huku akiwataka Watanzania
wacheze kwa wingi na mara nyingi ili wajiwekee mazingira mazuri ya
kuibuka mamilioni ya bahati nasibu ya Biko.
Mwisho
No comments:
Post a Comment