Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KUTOKANA na changamoto nyingi za ukosefu wa makazi ya
kuaminika kwa watu wengi, mshindi wa Sh Milioni 20, Innocent Nyeriga, amesema anatafakari
fedha zake alizokabidhiwa jana mjini Dodoma aziweke kwenye ujenzi wa nyumba.
Nyeriga mkazi wa Dodoma na mshindi wa Biko droo ya 29
iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, alikabidhiwa fedha zake
jana Jumatatu katika benki ya NMB, Mjini Dodoma tayari kwa kuanza kuzitumia kwa
matumizi yake ya kawaida.
Akizungumza kwa furaha kubwa, Nyeriga anayejighulisha na
kibarua cha kuhudumia mifugo mjini Dodoma, alisema kwamba lengo lake haswa ni
kujenga nyumba nzuri ili familia yake iondokane na changamoto ya ukosefu wa
makazi bora.
Shughuli ya makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wa Dodoma, Innocent Nyeriga ikiendelea katika benki ya NMB jana mjini Dodoma.Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kushoto akimkabidhi mshindi wao wa Sh Milioni 20 fedha zake jana Jumatatu katika benki ya NMB, Mjini Dodoma anayejulikana kwa jina la Innocent Nyeriga aliyeibuka kidedea kwenye droo ya 29
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa mjini
Dodoma, Innocent Nyeriga, akiwa amezilalia fedha zake baada ya
kukabidhiwa jana Jumatatu katika benki ya NMB, mjini Dodoma. Nyeriga
aliibuka mshindi wa Biko droo ya 29.
.
“Nawashukuru Biko bahati nasibu iliyokomboa maisha yangu,
hivyo fedha hizi tangu mwanzo nilizipanga nijengee nyumba saa chache baada ya
kupewa taarifa ya ushindi wangu, nikiamini haya yote yameletwa na Mungu kwa
kuwatumia Biko,” Alisema Nyeriga.
Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan
Melles, alisema mchezo wa Biko ni mzuri na rahisi kucheza pamoja na kushinda
kwake, huku akiwataka Watanzania kuchangamkia ili waweze kuvuna mamilioni ya
zawadi kwa kuanzia zile papo kwa hapo bila kusahau donge nono la Jumatano na
Jumapili la Sh Milioni 20 kama alizonyakua Nyeriga.
“Mchezo huu wa Biko unachezwa kwa kutumia simu za Tigo Pesa,
M-Pesa na Airtel Money ambapo wanachotakiwa ni kufanya miamala kuanzia Sh 1,000
na kuendelea, huku namba ya Kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.
“Mbali na kushinda zawadi kubwa ya Sh Milioni 20 ambayo ni
lazima iende kwa mshindi Jumatano na Jumapili, lakini pia zawadi za papo kwa
hapo zinatoka kila dakika ambazo ni zile za Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000,
100,000, 500,000 na Sh Milioni moja inayoenda kwa mshindi mara baada ya kupokea
ujumbe wa ushindi kwenye simu anayotumia kuchezea Biko,” Alisema Melles.
Kwa kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Dodoma, mshindi
mwingine wa Milioni 20 anatarajiwa kujulikana katika droo ya kesho Jumatano
maarufu kama Jumatamu na nyingine itakuwa Jumapili huku ikiitwa Jumadili na
waendeshaji hao wa Biko.
No comments:
Post a Comment