Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Sh Milioni 20 za Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu
ya Buku’, Irene Kitinga, amepokea fedha zake katika benki ya NMB, Tawi la Bank
House jijini Dar es Salaam, huku akisema kuwa ukitaka kujua nguvu ya mchezo huo
uibuke na ushindi.
Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles,
akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa Ubungo, jijini Dar es
Salaam, Irene Kitinga, katika benki ya NMB jana Jumatatu. Kushoto ni
Afisa wa NMB Tawi la Bank House Posta, jijini Dar es Salaam akishuhudia
makabidhiano hayo.
Irene mkazi wa Ubungo, jijini Dar es Salaam, alikabidhiwa
fedha zake juzi na Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko,
Hassan Melles, ikiwa ni siku moja tu tangu atangazwe mshindi kwenye droo ya 31
iliyochezeshwa jana.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Irene alisema kwamba
wengi hawaaamini kwamba fedha hizo hazitoki, jambo ambalo huthibitishwa sio
kweli mtu anapofanikiwa kuibuka na ushindi wa zawadi za Biko zinatoka kuanzia
Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, bila
kusahau donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko droo ya 31, Irene Kitinga, akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles kulia katika benki ya NMB Juzi Jumatatu.
Alisema hata yeye pia alidhani ni utani alipokuwa anapokea
simu ya Kajala Masanja, hivyo ni wakati wa kila mtu kucheza Biko ili ajiwekee
mazingira mazuri ya ushindi kama sehemu ya kutafuta fursa za kiuchumi kwa
kutumia mchezo wa Biko.
Mshindi wa Biko droo ya 31 Irene Kitinga akiwa amepozi kwa furaha baada
ya kupokea fedha zake kutoka Biko juzi katika benki ya NMB, jijini Dar
es Salaam jana.
“Ukitaka kujua thamani ya nguvu ya Buku ifike kwako, hivyo
kwangu mimi nawaasa Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi kucheza Biko,
maana hata kucheza kwake ni rahisi, kwa sababu baada ya kuingia kwenye kufanya
miamala kwenye simu za M-Pesa, Airtel Money na Tigo, huingiza namba ya Kampuni
ambayo ni 505050 na kumbukumbu namba 2456 tayari kwa kucheza Biko, huku kianzio
cha uchezaji kikiwa ni Sh 1,000 na kuendelea,” Alisema Irene.
Naye Melles, aliwataka Watanzania kuacha kucheza michezo
migumu, badala yake waitumie vyema Biko, maana kwa miezi mitatu ya Mei, Juni na
Julai pekee, tayari wameshalipa zaidi ya Sh Bilioni mbili kwa washindi wao
waliosambaa nchi nzima.
“Biko ni mchezo rahisi kucheza pamoja na kushinda kwake,
hivyo nawaomba kila mmoja acheze mara nyingi zaidi ili kujiwekea mazingira
mazuri ya ushindi, ukizingatia kuwa mbali na ushindi mkubwa wa Sh Milioni 20 unaotoka
Jumatano na Jumapili, pia zawadi za papo kwa hapo hutoka kila dakika moja,”
Alisema.
Mshindi mwingine wa droo kubwa ya Sh Milioni 20 anatarajiwa
kupatikana katika droo ya 32 itakayochezeshwa Jumatano, maarufu kama Jumatamu,
ikiwa ni mwendelezo wa mchezo wa biko kuendelea kusambaza mamilioni kwa
washindi wake katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment