Pages

Pages

Tuesday, August 22, 2017

Serikali yaipa somo TANESCO




Na Khalfan Said, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, pichani anayeongea amelitaka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanakamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusamabaza umeme kinachotarajiwa kujengwa huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kalemani ametoa maelekezo hayo leo Agosti 22, 2017, wakati alipofanya ziara kukagua miradi ya umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini, Kigamboni na eneo panapotarajiwa kujengwa kituo kingine cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Hakikisheni mradi wa uejenzi wa kituo hiki cha Kimbiji unakamilika ifikapo Machi 30, mwakani,(2018), na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni, chukueni mafundi waliokamilisha kazi ya kujenga kituo cha umeme kule Mtwara waje hapa, muwaache wale wanaojenga transition (njia ya kusafirisha umeme) wajenge, lakini wale mafundi wengine waleteni hapa ili mradi huu ukamilike.” Alifafanua.
 
Akiwa kwenye kituo cha kupoza na kusamabza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, Dkt. Kalemani aliipongeza TANESCO kwa juhudi kubwa walizofanya kwa hatua ujenzi waliyofikia ambapo sasa wameanza kufunga mashine kubwa. Kituo cha Kurasini ndicho kinachotegemewa sana na watu wa Mbagala, Kurasini na Kigamboni.
Ongezeko la haraka la wakazi kwenye maeneo ya Mbagala, na Kigamboni kumepelekea uhitaji mkubwa wa umeme ambapo umeme unaopatikana kwa sasa umekuwa haukidhi mahitaji ya wakazi wa maeneo hayo.
“Naomba niwaambie, mradi huu umechelewa sana, hivyo basi ongezeni kasi ili ifikapo Agosti 30, mwaka huu, mradi ukamilike nataka watu wa Mbagala, watu wa Kurasini, na watu wa Kigamboni wanaondokana na kero hii ya umeme, na mimi nitawaambia washeshimiwa wabunge wa Kigamboni Mheshimiwa Ndungulile (Dkt. Faustin Ndungulile) na Mheshimiwa Mangungu (Murtaza Magungu) Mbunge wa Mbagala kuhusu habari hii ili wawaambie wananchi wa maeneo haya wawe wavumilivu kwani mradi huu sasa utakamilika.” Alisema.
Dkt. Kalemani pia aliwaagiza viongozi wa TANESCO, kuhakikisha wanakusanya nguvu kwa maana ya vifaa kutoka ofisi zote za TANESCO mkoa wa Dar es Salaam, ili kuhakikisha wananchi wote wa Kigamboni wanaofikia 350 waliolipia ada za kuunganishiwa umeme wawe wamepelekewe umeme ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Agosti.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, aliwaambia waandishi wa habari kuwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu waziri yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuhakikisha kero hiyo inaondoka.
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam

 Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam
 Dkt. Kalemani (katikati), akitoa maagizo kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wa Kurasini.

Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (watatu kushoto), akimpatia maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha umeme cha Kigamboni, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto)
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), akiwa na  Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James, (kushoto), akiongea na waandishi wa habari.


Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo ambalo patajengwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula, (wapili kulia), akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo ambalo patajengwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani(katikati).
 Fundi wa TANESCO akiwa kazini pale Kigamboni
 Mhandisi Jahulula, (kushoto), akionyesha mahala mpaka wa eneo hilo la mradi unapoishia.
 Dkt. Kalemani (katikati), na viongozi wa TANESCO wakiwa kwenye eneo hilo la Kimbiji


No comments:

Post a Comment