Pages

Pages

Tuesday, August 22, 2017

Mohamed Kivugo: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba


Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia mwenye fulana ya Biko akimkabidhi fedha zake mshindi wao wa Bahati Nasibu, Mohamed Kivugo aliyeibuka kidedea katika droo ya 33 iliyochezeshwa Jumapili. Kushoto ni Afisa wa NMB, Tawi la Bank House, Posta jijini Dar es Salaam akishuhudia makabidhiano hayo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
FUNDI magari mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Mohamed Kivugo mwenye miaka 45, amesema kwamba fedha zake alizokabidhiwa jana baada ya kushinda kwenye Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', atazitumia kujengea nyumba ili aondokane na changamoto ya makazi.

Kivugo aliyasema hayo jana wakati anapokea zawadi ya Sh Milioni 20 za ushindi wa Biko alizokabidhiwa katika benki ya NMB,  tawi la Bank House Posta, jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko, Mohamed Kivugo akiwa ameshika fedha zake baada ya kukabidhiwa jana katika Tawi la NMB la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam tayari kwa matumizi yake ya kawaida.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kivugo alisema dhamira yake kubwa ni kutatua changamoto ya makazi kwa kuzitumia fedha za Biko kujenga nyumba. 

"Ingawa nimepata ushauri mzuri kutoka kwa watu wa NMB baada ya kukabidhiwa fedha zangu kutoka Biko baada ya kushinda kwenye droo ya 33 iliyochezeshwa Jumapili, lakini naamini wazo la nyumba ni zuri kwangu.
"Nawashauri Watanzania wenzangu wacheze Biko mara nyingi na wasikate tamaa ili waweze kuibuka na ushindi kama nilivyoibuka mimi, ukizingatia kuwa biko ni bahati nasibu inayotoa ushindi na kukabidhi fedha kwa Jataka, "Alisema.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles,  aliwataka Watanzania kucheza Biko ili wavune utajiri mkubwa kutoka kwenye bahati nasibu yao inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea katika Tigo Pesa, MPesa na Airtel Money huku namba ya Kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.

"Kushinda Biko ni rahisi pamoja na kupokea zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwenye simu za washindi wanazotumia kuchezea Biko bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 inayotoka kila Jumatano na Jumapili kama aliyoshinda mshindi wetu Kivugo wa Tabata," Alisema. 

Kwa mujibu wa Melles,  zaidi ya Sh Bilioni mbili zimelipwa kwa washindi katika miezi mitatu ya Mei, Juni na Julai, huku akiwataka Watanzania wacheze kwa wingi na mara nyingi ili wajiwekee mazingira mazuri ya kuibuka mamilioni ya bahati nasibu ya Biko.
Mwisho

No comments:

Post a Comment