https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, December 08, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Singida ateuliwa kuwa Katibu Mkuu Kilimo

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe pichani
Na Mathias Canal

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jan tarehe 07 Desemba, 2016 alifanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa mmoja na pia amefanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa kama ifuatavyo;



Dkt. Magufuli amemteua Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.
Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Mhandisi Mathew Mtigumwe anachukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Rais Magufuli amemteua Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia Mawasiliano. Dkt. Maria Sasabo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.
Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mhandisi Angelina Madete anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.
Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mhandisi Angelina Madete anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.Bw. Christopher Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Dkt. Rehema Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.
Dkt. Osward J. Mashindano anachukuwa nafasi ya  Bw. Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi nyingine 
Dkt. Osward J. Mashindano anachukuwa nafasi ya  Bw. Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi nyingine 







Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt. Osward J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...