Na Mwandishi Wetu, Riyadh Saudi Arabia
Maonesho makubwa ya kahawa na chocolate (coffee and Chocolate) yamemalizika kwa mafanikio jijini Riyadh Saudi Arabia, huku kwa mara ya kwanza maonyesho hayo yakishirikisha Ubalozi wa Tanzania, nchini Saudi Arabia. Katika maonyesho hayo yaliyoanza Desemba 20 hadi 23 mwaka huu, yalihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara wa Tanzania kwa nia ya kutangaza bidhaa za mazao ya kilimo na viwanda kutoka Tanzania.
Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa
Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, aliyasifu maonyesho hayo akisema
kuwa yamekuwa na tija kwa nchi ya Tanzania pamoja na wafanyabiashara
waliohudhuria. Alisema ofisi yake ilidhamilia kuyatumia maonyesho
hayo kwa ajili ya kutangaza bidhaa za Tanzania pamoja na wafanyabiashara wake
ili kufanikisha maendeleo yao kwa ujumla kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi
yao.
Mazungumzo yanaendelea kwenye banda hilo.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza mwenye suti nyeusi
alipata fursa ya kukutana na wawekezaji mbambali waliotembelea banda la
Tanzania wakati wa maonesho hayo.
Mfanyabiashara wa Tanzania aliyehudhuria maonyesho ya biashara ya Saudi Arabia, Bi Khadija Naif, akiwa na wasaidizi wake wakitoa maelekezo kwa watembeleaji wa banda lao.
“Tumeweka historia nchini Saudi Arabia kwa kuhakikisha kwamba tunashiriki kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuitangza nchi yetu, wafanyabiashara wetu pamoja na bidhaa zetu ili kila mmoja afahamua mazuri tuliyokuwa nayo. “Tulichofanya ni kuandaa banda letu lenye kila aina ya zuri letu hususan katika mazao ya kilimo ambayo kwa kawaida kila mtu alionyesha kuvutiwa na maonyesho hayo,” alisema H.E Mgaza.
Mazao mengine yaliyoonyeshwa katika maonyesho hayo ni pamoja na kahawa, chai, asali, katani, viungo, maziwa, mchele, karafuu, ufuta na nyinginezo huku mfanyabiashara Bi Khadija Naif akialikwa na Ubalozi ili kuwawakilisha wafanyabiashara kadhaa wa Tanzania kwa kubeba jukumu la kuleta bidhaa mbalimbali zilizooneshwa kwa siku hizo 4.
No comments:
Post a Comment