MAMBO FULANI MUHIMU
MAPENZI leo yamebadilika kwa kiasi kikubwa mno, maana baadhi
yao wameweka pesa mbele kuliko utu. Hao wanaishi na watu lakini hawapo mioyoni
mwao.
Dayna Nyange akiwa na Kala Jele 100. Pichaa hii si ishara kuwa wawili hawa wapo kwenye love hasa baada ya kukanusha vikali licha ya picha hii kunaswa mtandaoni.
Wanalala kitanda kimoja, lakini mioyo yao imejikunja kwa
kiasi kikubwa mno, jambo ambalo linashangaza. Mtu anaweza kujitia anacheka na
kufurahia hatua kwa hatua, lakini hana lolote.
Muongo mkubwa. Ni mwizi, maana kumbe huyo anayejifanya
anampenda, si kweli zaidi ya kugandishwa na fedha zao. Angalia mwenendo wa
vijana Dunia yaa leo.
Asilimia kubwa wanawapenda watu kutokana na uwezo wao
kifedha, namna gani wanawapa chochote kitu. Ndio hao wanapoingia kwenye
uhusiano na wenye nazo, hata kama wana pete za ndoa au uchumba, huzivua na kuziweka
kando.
Dunia ya leo ni pesa. Mapenzi ya kweli hakuna. Kijana
mdogo, lakini anatembea na mtu mwenye umri sawa na babu yake au baba yake, ila
anachoangalia yeye ni fedha tu.
Fedha ndio nini? Akishazipata anazitumiaje? Kwa bahati
mbaya, watu wa aina hii wanaamini fedha ndio kila kitu kwao. Pamoja na hayo,
watu walioendelea wanaamini fedha sio msingi wa maendeleo.
Na mtu anaweza kuwa na fedha, lakini akakosa furaha. Na hili
linadhihirika pale mtu anapofanya tendo la ndoa na mtu ambaye hamfurahii, yani hampendi
kutoka moyoni nwake.
Huyu hafurahii hata kama apewe Milioni moja. Ndugu msomaji
wangu, suala la tendo ni muhimu na ni jambo linalowaweka watu karibu na
kuonyesha namna gani uhusiano wao unasonga mbele.
Zamani haya mambo hayakuwapo. Na hata kama yalikuwapo, si
kwa kiasi hiki cha leo. Dunia ya leo pesa mbele kama tai. Ndio maana nimewahi
kuhoji huko kuwa sisi wote tujiangalie tuliokuwa nao kwenye uhusiano wa
kimapenzi wametupendea nini?
Je, wametupenda kutoka mioyoni mwao au ndio wanataka kuchuma
kutoka kwetu? Kuna msomaji wangu mmoja aliwahi kutaka ushauri wangu, akisema
ana uhusiano na mwanaume, ila anataka kumkubalia mwingine kwasababu anajiweza
na yule wake hana fedha.
Pia akasema huyo mwenye fedha zake si kama anampenda, ila
anataka tu apate fedha zake, ila pia anapata woga kuwa akiingia kwenye uhusiano
na huyo mwenye fedha zake yule anayempenda kwa dhati anaweza kumuacha na kukosa
yote.
Mengi alisema huyu dada akitaka kuonyesha ukweli wake,
lakini nilipomwambia huyu mwanaume mwenye fedha chochote atakachotaka utakuwa
radhi?
Hakuwa na jibu la moja kwa moja, ila nilipata ushahidi kuwa
katika mitaa, jamii yetu, wapo wasichana ambao hao huenda hawafurahii pia tendo
la ndoa, hasa kama wanajiingiza kwenye uhusiano na wanaume ambao hawapo moyoni
mwao.
Ili ufurahie tendo la ndoa kwanza lazima unayefanya naye
umridhie kutoka moyoni mwako. Kila anachokifanya, anachokitaka, wewe mhusika
uwe tayari, hasa kama ni chaguo lake.
Lakini kujilazimisha kwasababu ya fedha, ina maana bado
huwezi kufurahia mapenzi. Kwa lugha ya kawaida, mtu wa aina hii ni kama vile
amelazimishwa tendo la ndoa, yani ameingiliwa kimwili bila ridhaa yake, eti
kwasababu eneo hilo kuna mpunga.
Ndio hawa wanawasaliti wanaume wao, wake zao kwasababu kuna
mahali wanapewa fedha. Ni ajabu na kweli. Je, ni wangapi tunatembea na watu
tusiowapenda kwasababu ya fedha zao?
Ukiacha hizo fedha zao ambazo wengi wao huzitoa na baadaye
kuwanyanyasa, ni faida gani nyingine zinazopatikana, ukizingatia kuwa
umeshajidhalilisha kwa kibosile huyo?
Sitaki kuelezea magonjwa pia yanayoweza kupatikana, maana
wenye fedha wengi wana uwezo wa kutembea na kila wanayemtaka, hasa kama atakuna
na warahisi, ukiwapo wewe unayeona una kila sababu ya kuanza uhusiano na wenye
nazo. Tamaa zilimshinda fisi.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment