Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa
Morogoro
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi
kipya, maarufu kama Bongo Fleva, Ahmad Ally Madee, amesema kuwa hajawahi kuona
ugomvi mzito kati ya marehemu Albert Mangweha Ngwair na msanii mwingine
Tanzania.
Madee akiingia Uwanja wa Jamhuri kumuaga marehemu Ngwair, aliyozikwa Alhamisi mkoani Morogoro.
Madee aliyasema hayo mkoani
Morogoro katika mazishi ya Ngwair, yaliyofanyika katika Makaburi ya Kihonda
Kanisani na kuhudhuriwa na watu wengi, yakitanguliwa na shughuli ya kuaga
Uwanja wa Jamhuri.
Akizungumza kwa masikitiko
makubwa, Madee alisema kuwa hajawahi kuona ugumvi mzito wa Ngwair na wasanii
wengine, hivyo inaonyesha namna gani maarehemu aliishi kwa upendo.
Alisema katika sanaa kumekuwa
na migogoro ya hapa pale, lakini kama Ngwair aliweza kugombana na watu, basi
ilikuwa kimya kimya, kama alivyowahi kuimba enzi za uhai wake.
“Simsifii Ngwair kwasababu leo
ametangulia mbele ya haki, ila kwakweli Tanzania tumepoteza msanii nyota na
aliyekuwa na uwezo wa aina yake, huku
kila mmoja akimpenda na kumheshimu sana.
“Zaidi ni jinsi alivyoweza
kuishi kwa upendo na wasanii wote, ukizingatia kuwa sisi kwenye fani hii wakati
mwingine unalumbana na mtu, lakini kwa Ngwair yeye hilo suala sijawahi
kulisikia,” alisema Madee.
Madee anayetesa na wimbo wa
Pombe Yangu, pia ni Rais wa kundi la Tip ‘Connection’ lenye maskani yake
Manzese jijini Dar es Salaam, akijulikana pia kwa jina la Rais wa Manzese.
No comments:
Post a Comment