Pages

Pages

Sunday, June 09, 2013

Pesa zimekuja kuondoa mapenzi ya kweli kwa binadamu duniani



MAMBO FULANI MUHIMU

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAPENZI leo yamebadilika kwa kiasi kikubwa mno, maana baadhi yao wameweka pesa mbele kuliko utu. Hao wanaishi na watu lakini hawapo mioyoni mwao.
Dayna Nyange akiwa na Kala Jele 100. Pichaa hii si ishara kuwa wawili hawa wapo kwenye love hasa baada ya kukanusha vikali licha ya picha hii kunaswa mtandaoni.

Wanalala kitanda kimoja, lakini mioyo yao imejikunja kwa kiasi kikubwa mno, jambo ambalo linashangaza. Mtu anaweza kujitia anacheka na kufurahia hatua kwa hatua, lakini hana lolote.

Muongo mkubwa. Ni mwizi, maana kumbe huyo anayejifanya anampenda, si kweli zaidi ya kugandishwa na fedha zao. Angalia mwenendo wa vijana Dunia yaa leo.

Asilimia kubwa wanawapenda watu kutokana na uwezo wao kifedha, namna gani wanawapa chochote kitu. Ndio hao wanapoingia kwenye uhusiano na wenye nazo, hata kama wana pete za ndoa au uchumba, huzivua na kuziweka kando.

Dunia ya leo ni pesa. Mapenzi ya kweli hakuna. Kijana mdogo, lakini anatembea na mtu mwenye umri sawa na babu yake au baba yake, ila anachoangalia yeye ni fedha tu.

Fedha ndio nini? Akishazipata anazitumiaje? Kwa bahati mbaya, watu wa aina hii wanaamini fedha ndio kila kitu kwao. Pamoja na hayo, watu walioendelea wanaamini fedha sio msingi wa maendeleo.

Na mtu anaweza kuwa na fedha, lakini akakosa furaha. Na hili linadhihirika pale mtu anapofanya tendo la ndoa na mtu ambaye hamfurahii, yani hampendi kutoka moyoni nwake.

Huyu hafurahii hata kama apewe Milioni moja. Ndugu msomaji wangu, suala la tendo ni muhimu na ni jambo linalowaweka watu karibu na kuonyesha namna gani uhusiano wao unasonga mbele.

Zamani haya mambo hayakuwapo. Na hata kama yalikuwapo, si kwa kiasi hiki cha leo. Dunia ya leo pesa mbele kama tai. Ndio maana nimewahi kuhoji huko kuwa sisi wote tujiangalie tuliokuwa nao kwenye uhusiano wa kimapenzi wametupendea nini?

Je, wametupenda kutoka mioyoni mwao au ndio wanataka kuchuma kutoka kwetu? Kuna msomaji wangu mmoja aliwahi kutaka ushauri wangu, akisema ana uhusiano na mwanaume, ila anataka kumkubalia mwingine kwasababu anajiweza na yule wake hana fedha.

Pia akasema huyo mwenye fedha zake si kama anampenda, ila anataka tu apate fedha zake, ila pia anapata woga kuwa akiingia kwenye uhusiano na huyo mwenye fedha zake yule anayempenda kwa dhati anaweza kumuacha na kukosa yote.

Mengi alisema huyu dada akitaka kuonyesha ukweli wake, lakini nilipomwambia huyu mwanaume mwenye fedha chochote atakachotaka utakuwa radhi?

Hakuwa na jibu la moja kwa moja, ila nilipata ushahidi kuwa katika mitaa, jamii yetu, wapo wasichana ambao hao huenda hawafurahii pia tendo la ndoa, hasa kama wanajiingiza kwenye uhusiano na wanaume ambao hawapo moyoni mwao.

Ili ufurahie tendo la ndoa kwanza lazima unayefanya naye umridhie kutoka moyoni mwako. Kila anachokifanya, anachokitaka, wewe mhusika uwe tayari, hasa kama ni chaguo lake.

Lakini kujilazimisha kwasababu ya fedha, ina maana bado huwezi kufurahia mapenzi. Kwa lugha ya kawaida, mtu wa aina hii ni kama vile amelazimishwa tendo la ndoa, yani ameingiliwa kimwili bila ridhaa yake, eti kwasababu eneo hilo kuna mpunga.

Ndio hawa wanawasaliti wanaume wao, wake zao kwasababu kuna mahali wanapewa fedha. Ni ajabu na kweli. Je, ni wangapi tunatembea na watu tusiowapenda kwasababu ya fedha zao?

Ukiacha hizo fedha zao ambazo wengi wao huzitoa na baadaye kuwanyanyasa, ni faida gani nyingine zinazopatikana, ukizingatia kuwa umeshajidhalilisha kwa kibosile huyo?

Sitaki kuelezea magonjwa pia yanayoweza kupatikana, maana wenye fedha wengi wana uwezo wa kutembea na kila wanayemtaka, hasa kama atakuna na warahisi, ukiwapo wewe unayeona una kila sababu ya kuanza uhusiano na wenye nazo. Tamaa zilimshinda fisi.
0712 053949
0753 806087

No comments:

Post a Comment