Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu mwenye miwani, akichanganya udongo katika ufyatuaji wa matofali.
Na Kambi
Mbwana, Handeni
MKUU wa
wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amezindua ufyatuaji wa matofali katika
Shule ya Msingi Kwedikabu, yenye wanafunzi 540, huku ikiwa na vyumba viwili vya
madarasa na kusababisha idadi kubwa kusomea nje.
Uzinduaji
huo aliufanya mwishoni mwa wiki akiwa na wananchi wengi katika kijiji hicho kwa
ajili ya kufanya kazi hiyo kwa umoja na kuweza kuwakomboa wanafunzi wa shule
hiyo yenye changamoto nyingi, ikiwamo ya kosomea nje.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, kushoto akizungumza na wanakijiji wa Kwedikabu, baada ya kuzindua ufyatuaji wa matofali wa shule ya kijiji hicho.
Akizungumza
katika uzinduaji huo shuleni hapo, Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo
Rweyemamu, alisema shule ni mali ya watu wote, hivyo wananchi wanatakiwa
wachangie kwa hali na mali ili watoto wao wasomee sehemu nzuri.
Alisema
kuamua yeye kuingia katika shimo la tope na kuponda udongo ni kuonyesha kuwa
kazi hiyo inahitaji ushirikiano na kufanya kazi kwa moyo wote, ukizingatia
kwamba watoto wao wanasomea nje huku wazazi wao wakiangalia kwa macho.
“Hatuwezi
kwenda hivi kwa kuangalia watoto wakisomea nje wakati wazazi tupo, ndio maana
nimekuja kwa ajili ya kushiriki kikamilifu ufyatuaji wa matofali haya, nikijua
pia shughuli hii itaendelea wakati wote.
“Kijiji
kinaingia aibu, maana watoto wao wanasomea nje na kushuhudia utoro mwingi,
maana kipindi cha mvua, hakuna motto anayekubali aende shule akapigwe na mvua,
badala yake kuamua kulala tu nyumbani,” alisema Rweyemamu.
Mbali na ufyatuaji wa matofali, DC Muhingo pia ameitumia
fursa hiyo kuzungumza na wananchi juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa
ushirikiano, sambamba na kuwa makini na ardhi yao inayowaniwa na watu wenye nia
ya kujineemesha kwa kuwalaghai na visenti vya kula.
No comments:
Post a Comment