Tino Muya
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKALI
wa filamu hapa nchini, Tino Muya, kesho Ijumaa anatarajia kuizundua filamu yake
mpya ya mapigano, inayojulikana kama (CID), katika Ukumbi wa Biashara Complex.
Filamu
hiyo imeandaliwa kwa kiwango cha juu, huku ikiwa ya kwanza kwa msanii huyo
kucheza filamu za mapigano, ukizingatia kwamba kwa muda mrefu amekuwa akicheza
zile zinazoelezea uhusiano wa kimapenzi tu.
Akizungumza muda mfupi na HANDENI KWETU, Tino alisema kwamba filamu hiyo ipo kwenye ubora wa hali ya juu, huku akipanga
kuizindua Ijumaa katika Ukumbi wa Biashara Complex, Kijitonyama.
Alisema
wadau na mashabiki wa filamu watapata kutu kizuri kutoka kwake, akiandaa chini
ya Kampuni yake ya Tino Muya Films Company, aliyoanzisha mwaka 2009 kwa ajili
ya kujihusisha na sanaa hapa nchini.
“Ni
matarajio yangu kuwa watu watapata kitu kizuri kutoka kwangu, huku nikiachana
kabisa na filamu za mapenzi kwa ajili ya kubadilisha soko la filamu hapa nchini
kutoka mapenzi hadi mapigano.
“Naamini
wadau na mashabiki watakuja kwa wingi kujionea jinsi gani watu wanaingia katika
ulimwengu mpya wa filamu, maana wasanii wengi na waandaaji wamekuwa
wakitayarisha filamu za kimapenzi tu,” alisema Tino.
Filamu
nyingine zilizoaandaliwa na kampuni hiyo ni pamoja na Hatia, Shoga Yangu,
Nzowa, One Blood, Hazard, My Heart, Olopong, Means Day Out, End of the Day,
Good Fellow, Rooleen na sasa CID, filamu ambayo imeandaliwa kwa ufanisi kwa nia
ya kuleta mapinduzi kisanaa.
No comments:
Post a Comment