Mchezaji wa tenisi, Mohamed Dewji
Mchezo wa tenisi ni mzuri mno lakini wengi wanaoingia humo
ni wale ambao wazazi wao wana chochote kitu. Sababu inayosababisha hilo ni namna ya mchezo
wenyewe pamoja na vifaa vyake kuuzwa bei ghari mno.
Mtu ambaye hata kula yao
nyumbani ni tabu, hawezi kutumia kiasi kikubwa cha pesa kununulia vifaa hivyo
vya mchezo wa tenisi. Pichani ni mcheza tenisi, Mohamed Dewji, kama alivyokutwa
na mpiga picha mahiri wa michezo, Rahel Pallangyo, leo katika Viwanja vya
Gymkhana, jijini Dar es Salaam.
Ipo sababu ya wadau kuliangalia suala hilo
ili kuufanya mchezo huo ni wa watu wote badala ya wale wenye nazo, zikiwamo
sura nyeupe kwa Tanzania.
Wakati nasema hayo, soka ndio mchezo pekee kwa Tanzania ambao unavutia kuchezwa na
kila mtu.
Kwa maoni na ushauri
kambimbwana@yahoo.com
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment