Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Milovan Cirkovic, leo
anatarajia kuanika chanzo cha sare yake na Coastal Union
ya Tanga pamoja na muendelezo wa ligi hiyo, huku wakikipiga na Kagera Sugar,
kesho katika Uwanja wa Taifa.
Kutoka sale na Coasta Union kumepokelewa kwa shingo upande
na mashabiki wa timu hiyo, hasa wale waliokwenda kuishuhudia mechi hiyo ya aina
yake na kuipatia Simba pointi moja, hivyo kufikisha pointi 17.
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga
Simba wanaingia uwanjani kucheza na Kagera Sugar huku wakiwa
na machungu ya kusimamishwa na Wagosi wa Kaya, licha ya kujipanga kwa ajili ya
mchezo huo uliohudhuliwa na mashabiki wengi wa jijini Tanga na maeneo mengine
ya nchi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa
Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kocha huyo atazungumza yote yaliyosababisha
asihndwe kupata pointi tatu kutoka kwa Wagosi wa Kaya, mechi iliyopigwa
Jumamosi, katika Uwanja wa Mkwakwani.
Alisema kwamba anaamini kwa kujua mapungufu yake, ni sababu
ya kuwaamisha mashabiki wake kuwa watashinda mbele ya Kagera Sugar wanaotoka
mjini Bukoba na kuikuta Simba yenye machungu na mchezo huo.
“Simba tuna uchungu na mechi hiyo ya Kagera Sugar, ila
sitaki kuzama sana
kwenye mambo ya kiufundi maana yataongelewa na kocha wetu kwa ajili ya kuwatoa
hofu mashabiki na wanachama wote hapa nchini.
“Naamini kuna mengi yametokea na yatatokea katika ligi hii
yenye ushindani wa aina yake, lakini huenda limepatia ufumbuzi na kocha wetu,
Milovan hivyo kuendeleza wimbi la ushindi na hatimae kunyakua ubingwa kwa mara
ya pili mfululizo,” alisema Kamwaga.
Ligi ya Tanzania Bara imezidi kuwa na ushindani wa aina
yake, huku kila timu ikipania kushinda katika mechi zake zote, jambo
linalozifanya timu kongwe za Simba na Yanga zitumie nguvu kubwa ili kuzipa
ushindi.
No comments:
Post a Comment