MABONDIA mbalimbali wa uzito wa juu hapa nchini, wanatarajia
kukutanishwa Jumamosi na kufanya mazoezi ya pamoja, huku wakishuhudiwa na mmoja
wa wafadhili wa Evender Hollfied, Andrew Jowel.
Kufanya mazoezi kwa pamoja ni sehemu ya kufanya mchakato wa
kujitafutia mafanikio makubwa katika sekta ya masumbwi na kuinua kiwango cha
mchezo huo hapa nchini.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,
muandaaji wa tukio hilo, ambaye pia ni bondia
mahiri hapa nchini, Japhet Kaseba, alisema lengo ni kutathimini namna ya
kuendeleza mchezo wa masumbwi Tanzania.
Japhet Kaseba
Alisema anaamini mabondia watakaofika siku hiyo katika kambi
ya ngumi ya Kaseba, iliyopo Mwananyamala jijini Dar es
Salaam watakuwa na mwamko zaidi wa kufikia malengo yao.
“Tayari mabondia mbalimbali wanajua kuwa tutakuwa na mgeni
huyo aliyekuja kutembelea Tanzania,
huku akiwa anajua mambo mengi yanayohusu mchezo wa masumbwi duniani.
“Kuanzia saa tisa alasiri, mabondia wote tutaanza mazoezi ya
pamoja katika gym yangu, hivyo kila anayependa kushiriki afike maana lengo ni
kuangalia namna ya kujitangaza na kuonyesha kwamba Tanzania wapo mabondia wenye vipaji
na dhamira ya kweli ya kufika mbali,” alisema Kaseba.
Kaseba ni miongoni mwa mabondia wenye mafanikio makubwa
katika mchezo wa masumbwi, huku akiogopwa na mabondia wakali wanaoshindwa kucheza
naye kila anapojitokeza promota wa kumkutanisha nyota huyo ambaye pia aliwahi
kuwa bingwa wa Dunia wa Kick Boxing.
No comments:
Post a Comment