Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII wawili wa filamu wenye majina makubwa hapa nchini,
Wema Sepetu na mwenzake Aunt Ezekiel wamewaangukia Watanzania kwa kusema hawajajua
kama watawakera watu haswa baaada ya picha zao
kuzagaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari.
Wema na Aunt walipokuwa katika ziara ya tamasha la Fiesta,
walipigwa picha za utupu, walipokuwa jukwaani hivyo kuwakera watu wengi, ukizingatia
kwamba wao ni kioo cha jamii na wanastahili kuishi kwa staha na sio kuanika
nyeti zao.
Wema Sepetu akiomba radhi kwa Watanzania
Wema na Aunt Ezekiel waliitumia siku ya jana katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuzungumza na waandishi wa habari, ili wafikishe vilio vyao, wakisindikizwa na Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAF), Willsona Makubi pamoja na msanii mwingine wa fgilamu, Tino Muya.
Akizungumzia sakata hilo,
Wema alisema hawana uzoefu wa kupanda katika majukwa makubwa, hivyo baada ya
kufanya hivyo, baadhi ya wapiga picha na wananchi wengine waliingia kwenye kazi
hiyo na kusambaza picha zao.
“Sikujua kabisa kama picha zangu zingezagaa kwenye mitandao
maana sina uzoefu huo kama waliokuwa nao
wasanii wengine wa muziki wanaopanda jukwaani kila wakati, ila kwa sasa nimejua
na naamini sitawakera tena Watanzania.
“Nipo chini ya miguu yao
na mkawaeleze kwamba tabia yangu inawachosha pia hata ndugu zangu, maana nao ni
waathirika kwakuwa wanazipata kwenye vyombo vya habari na jinsi
ninavyoonyeshewa vidole,” alisema Wema.
Naye Aunt alisema tangu sasa amekuwa msanii mpya naa kioo
cha jamii, maana atajilinda katika kila jambo analofanya ili aendelee
kuheshimiwa na kutumainiwa kama msanii mwenye
dhamana na kutangaza utamaduni wa Mtanzania.
Huku akiwa na masikitikio makubwa, Aunt alisema,“ Hata mimi
na mwenzangu Wema tunapata tabu sana,
hivyo tuliamua kukutana na viongozi wetu ili tutumie fursa hii kuzungumza na
nyie tukijua fika mtafikisha vilio vyetu kwa Watanzania wote,” alisema
mwanadada huyo ambaye jana alivaa vazi la heshima na kuahidi kuwa mtu mwenye
maadili.
Akielezea sakata hilo, Makubi
alisema wanaamini wasanii hao watafuata maadili ya Mtanzania katika kujiheshimu
katika maisha yao yote, ndio maana baada ya
tabia zao kuwa mbaya waliamua kujishusha na kutaka suluhu na jamii yao.
“Wasanii hawa wasamehewe na naamini watakuwa watu wenye
maadili kuanzia hapa, hivyo ni jukumu letu kujua kuwa kadri siku zinavyokwenda
wanazidi kupanuka kiakili na kujua wataacha tabia zao za kukera,” alisema.
Katika tamasha la Fiesta liliiofanyika katika mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara, wasanii hao waliambatana kwenye ziara hiyo na
kupanda jukwaani kuwasalimia mashabiki wao, jambo ambalo hata hivyo liliwakera
baadhi ya watu baada ya kupanda na vivazi vya utupu na kujiachia jukwaani hivyo
kupigwa picha mbaya.
No comments:
Post a Comment