Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Shindano
kabambe la kumsaka Mfalme wa Mic (The Mic King), litapambwa na wakali wa Bongo
Fleva, Said Juma ‘Chegge’ na Amani James Temba ‘Mheshimiwa Temba’.
Kila
kitu kuhusu shindano hilo ambalo mshindi wake
atajinyakulia zawadi ya gari la kifahari ni Jumapili hii kwenye Ukumbi wa Dar
Live, Mbagala Zakhem, Dar es Salaam.
Mratibu
wa Shindano la The Mic King, Luqman Maloto amesema kuwa sambamba na Chegge
pamoja na Temba, bi. Mkubwa anayetamba kwa sasa kwenye ulingo wa Bongo Fleva,
Bi. Cheka, naye atakuwepo.
“Siku
hiyo, kutakuwa na shoo maalum kwa wakali wapya kutoka timu ya Mkubwa na Wanawe
kutambulishwa chini ya Meneja Said Fella ‘Mkubwa’,” alisema Luqman na kuongeza:
“Vilevile
Bendi ya Extra Bongo ikiongozwa na Ally Choki, Banza Stone, Khadija Mnoga
‘Kibotel’ na Rogert Hegga ‘Katapila’, itakuwepo kufanikisha siku hiyo nzuri.”
Luqman
aliongeza kuwa Jumapili iliyopita, walisakwa vijana 12 kutoka Temeke, wiki hii
ni zamu ya Wilaya ya Ilala, nayo kushindana na kupata 12 Bora yao.
“Niwasihi
tu mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani msisimko tuliouona mwanzoni ulikuwa si
wa kitoto. Ikumbukwe kwamba mshindi atajiondokea na gari la kifahari,” alisema
Luqman.
No comments:
Post a Comment