Ibrahimu Mawe
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
BONDIA Ibrahimu Mawe, maarufu kama 'King Class Mawe',
anatarajia kuingia kambini mwishoni mwa wiki hii kujiandaa na kujiandaa na
pambano lake na Said Mundi, anayetokea Tanga, kwa Wagosi wa Kaya, litakalopigwa
Desemba 9, katika Ukumbi wa PTA, Sabasaba, jijini Dar es Salaam na kusubiriwa
kwa hamu na mashabiki wa ngumi.
Maandalizi ya Class Mawe, yanakuja siku chache baada ya
kushinda katika patashika yake na Jonas Segu wa Dar es salaam, aliyempiga na kuwafurahisha
mashabiki wake katika mchezo huo wa masumbwi hapa nchini.
Akizungumza mapema leo mchana jijini Dar es Salaam, kocha wa mchezo wa
masumbwi, Rajabu Mhamila, maarufu kama ‘Super D’, amesema bondia huyo atakuwa
katika mikono yake kwa ajili ya kujiandaa na pambano hilo.
Alisema bondia wake ataanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa
na pambano hilo
muhimu, akiwa na lengo la kufanya vizuri zaidi katika mchezo wa masumbwi na
kurithi mikoba ya wapiganaji wengine waliotamba hapa nchini.
“Naomba wadau wampe sapoti kijana huyu katika pambano lake lijalo,
ukizingatia kwamba nia ni kuhakikisha kuwa anapiga hatua zaidi katika mchezo wa
masumbwi hapa nchini na kufikia malengo ya wakali wengine.
“Naamini kila kitu kitakuwa sawa, ndio maana Class ataingia
kambini mapema kwa ajili ya kumnoa vizuri ili awe nyota na kutikisa katika
ulingo wa masumbwi na kuupandisha chati kama
wadau tunavyopania,” alisema.
Ibrahim Class ni miongoni mwa mabondia wanaochipukia kwa
kasi hapa nchini, huku akiwa na mipango imara ya kuwachapa wapinzani wake
katika mapambano mbalimbali yanayoandaliwa kwa ajili ya kuonyesha cheche zake.
No comments:
Post a Comment