Kalala Junior akiwaimbisha mashabiki wa Twanga Pepeta
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi hapa nchini ya The African Stars,
Twanga Pepeta, jumapili inatarajia kufanya shoo ya aina yake, waliyoipa jina la
Facebook Fans, itakayofanyika katika Ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama.
Kufanyika kwa shoo hiyo ni kuwaweka sawa na kuwakumbuka
mashabiki wao wanaoendelea kuwaunga mkono kwa miaka 11 sasa walipoanzisha bendi
hiyo inayopendwa na watu wengi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa ASET,
Hassan Rehani, alisema mashabiki wao wote, wakiwamo waandishi wa habari na wadau
wengine watakumbukwa na kuthaminiwa mchango wao.
Alisema kwamba bendi yao
imekuwa ikipita katika vipindi mbalimbali, hivyo wanaamini mafanikio yao kwa sasa yamesababishwa
na watu wengi, jambo linalowafanya waandae part hiyo hiyo usiku wa facebook na
Twanga.
“Tumekuwa tukifanya vizuri katika soko la muziki wa dansi
kutokana na mchango wa kila mmoja wetu, hivyo naamini wadau wote tutakutana
katika Ukumbi huo wa Mzalendo na kucheza pamoja kisigino.
“Twanga ni bendi ya kila mmoja, hivyo nadhani changamoto
zinazoonekana kwa sasa ni sehemu ya kutufanya tuwe juu zaidi, huku tukiamini
kada mbalimbali na jinsi tofauti tutakutana ili tucheze pamoja,” alisema.
Twanga Pepeta ipo chini ya Luiza Mbutu pamoja na waimbaji
mbalimbali wenye uwezo wa juu, akiwamo Kalala Junior aliyejiunga na bendi yake
hiyo, akitokea Mapacha Watatu na maswahiba zake, Jose Mara na Khalid Chokoraa,
huku Ally Akida, Chokoraa, Soud Mohammed au MCD na wengineo wakithibitisha
kushiriki katika onyesho hilo kutokana na kuwahi kufanya kazi na bendi hiyo kwa
nyakati tofauti.
No comments:
Post a Comment