Mpe moyo, usimkatishe tamaa
Wawili wapendanao.
MAMBO FULANI MUHIMU
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NI dhahiri kila mtu ana mapungufu yake katika
suala zima la uhusiano wa kimapenzi.
Sio wote ni wajuzi wa mambo. Sio wote wanaelewa
wapi kwa kuwashika wenzao, hadi wajisikie raha katika suala la mapenzi.
Kila mtu na utundu wake. Wapo ambao ni wazito
kabisa, wakikosa mbinu nzuri zinazoweza kustawisha mapenzi yao kwa wale waliowapenda.
Ndio, maana watu hao husubiri hulka na utundu wa
wenzao tu, wakitaka waendeshwe kwa kila hatua. Waambiwe simama, inuka, lala au
fanya hivi!
Bila kuendeshwa, kamwe hawawezi kung’amua wenyewe
na kubuni yale yanayoweza kuwapa raha wenzao. Hayo ndio ya kujadili leo.
Naamini nitaweza kutoa darasa japo kwa kiasi
kidogo, huku nitarajia kujibu maswali yako, hasa kama
sitaingia moja kwa moja, kutokana na sababu za kimaadili, maana gazeti
linasomwa na watu wengi, wakubwa na watoto.
Nimeamua kusema haya, huku nikijua fika, ingawa
baadhi yao ni
wazito, lakini wachache wao hupenda kujifunza na kuwagurahisha wapenzi wao.
Ni kutokana na hilo, kuna kila sababu ya kuwapa moyo, pale
tutakapogundua kwamba kwa siku hiyo, wapenzi wetu wamejituma, kukazana na
kufanya yale yaliyotupa raha na amani katika uhusiano wetu.
Tusiwanyanyase na kuwaona bado ni mizigo. Tuone
kama walioamua kuwa na sisi kwa raha na tabu, ndio maana wanaamua kujitoa kwa
moyo.
Kuna watu ambao hujikuta wakitoa matamshi makali
kwa wapenzi wao. “Huna lolote, bado mgeni kwenye ulimwengu wa mapenzi na
mengineyo.
Kuna mtu aliwahi kulalamika juu ya
jambo hili. Dada huyo alisema, “sijawahi kusifiwa hata siku moja na kila siku
naambiwa sifai”.
Kwa sababu hiyo, dada huyo alijikuta akihoji labda
hayupo moyoni kwa mwanaume huyo, ambaye kwa hakika yeye amempenda na kuamua
kujitoa kwake.
Sawa, lakini hapa udhaifu upo kwa mwanaume. Nasema
hivyo, maana hajui harakati na jinsi gain wasichana wanatakiwa kupikwa kadri
unavyotaka wawe.
Haya utayafanya siku chache baada ya kuingia naye
kwenye makubaliano ya kuanzisha mapenzi, hivyo hakuna haja ya kuwaona si lolote
si chochote.
Kama wewe ni hodari wa mapenzi, pia una wajibu wa
kuelewa, si wote ni wajuzi, huku pia ukiwa mwepesi wa kumsifia mwenzako katika
siku zote za uhusiano wenu, hasa kama amefanya
kitu cha tofauti.
Kama leo unaona kabisa mpenzi wako amefanya jambo
geni, kwanini usimsifie ili aongeze bidii? Haina haja ya kumuona mgeni kila
wakati.
Kama
mabadiliko yapo, ni wakati wako wa kuona kumbe uliyekuwa naye, angalau anaumiza
kichwa, kuwaza namna ya kukutosheleza.
Anafanya hivyo maana hataki akukose. Hataki kuona
unakuwa na uhusiano mpya kila wakati, ukizingatia kwamba wapo wanaoanzisha
uhusiano mpya kwa kisingizio kuwa wapenzi wao, wake au waume zao
hawawatoshelezi katika mambo fulani muhimu.
Huo ndio ukweli wa mambo, Tunapaswa kuwa makini
kwa ajili ya kulinda, kudumisha na kustawisha uhusiano wetu, maana hapo ndipo
utamu wa mapenzi unapoanzia na kushika kasi siku zote.
Tukutane wiki ijayo.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment