Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia, maarufu kama Wazee
wa Ngwasuma, wanatarajia kufanya shoo ya nguvu katika Ukumbi wa Hill Take,
uliopo Ukonga, jijini Dar es Salaam,
Ijumaa ya Oktoba 19.
Kuvamia ukumbi huo ni sehemu ya kuwapatia burudani mashabiki
wao wa Ukonga, wakiamini kuwa litaacha watu hoi kutokana na mipango yao waliyoiweka kwa ajili
ya kufanya shoo ya nguvu na kuwaburudisha mashabiki wao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam na Handeni Kwetu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema kwamba mipango kwa ajili ya shoo hiyo
imekamilika kwa ajili ya kuwapatia raha mashabiki wao wa Ukonga.
Alisema bendi yao
imekuwa ikitamba na nyimbo mbalimbali zinazopendwa na watu wengi, hivyo
anaamini mashabiki wao watapata raha za aina yake na kuendelea kuwaunga mkono
katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.
“Ni bendi yenye mipango imara katika tasnia ya muziki wa
dansi, hivyo naamini mashabiki wetu watakuja kwa wingi katika ukumbi huo kwa
ajili ya kucheza na Wazee wa Ngwasuma wenye nyimbo zinazopendwa na wengi.
“Nyimbo kama ‘Heshima kwa Mwanamke’, ‘Otilia’ na nyinginezo
ni kati ya zitakazoporomoshwa na waimbaji wetu, hivyo naaamini mashabiki
watakuja kwa wingi kuburudika pamoja na kudhihirisha FM Academia ni zaidi yao,” alisema Mkinga.
FM Academia ipo chini ya Rais wa Vijana, Nyosh Al Sadaat,
akiwa sambamba na wakali wengine akiwamo Patchou Mwamba, ambaye pia ni mkali
katika tasnia ya filamu baada ya kushiriki katika filamu mbalimbali hapa
nchini.
No comments:
Post a Comment