BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo, kesho Ijumaa,
wanatarajia kufanya shoo ya nguvu katika Ukumbi wao wa nyumbani wa White House,
Kimara Korogwe, jijini Dar es Salaam.
Burudani hizo zitaongozwa na Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally
Choki, sambamba na wakali wengineo wanaofanya vyema katika tasnia ya muziki wa
dansi hapa nchini.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,
Choki alisema kwamba shoo yao
hiyo itapambwa na wakali wao wote, akiwamo Rogert Hega 'Catapiler', Ramadhani
Masanja ‘Banza Stone’ na Khadija Mnoga 'Kimobitel'.
Alisema kuwa usiku huo wa kizazi cha dansi utawahusisha
wanamuziki hao walio na bendi hiyo katika maonyesho yatakayofanyika kweye kumbi
Bongo Resort na Meeda Sinza.
Baadhi ya nyimbo zao ni 'Kila Chenye Mwanzo', 'Game 111',
'Nguzo Tano', 'Mtaji wa Maskini', 'Elimu ya Mjinga', 'Simba Ananguruma', 'Kumekucha',
'Mtu Pesa', 'Password',' Chuki Binafsi', 'Jirani', 'Umbeya hauna Posho',
'Fadhila kwa Wazazi' 'Mtenda Akitendewa', 'Mjini Mipango' na nyinginezo.
Aidha, onyesho hilo pia linatarajiwa kupambwa na kikundi cha burudani cha Baikoko na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Husein Machozi ambaye atakuwa anatambulisha wimbo wake mpya.
Aidha, onyesho hilo pia linatarajiwa kupambwa na kikundi cha burudani cha Baikoko na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Husein Machozi ambaye atakuwa anatambulisha wimbo wake mpya.
No comments:
Post a Comment