Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama cha
Wamiliki wa Malori Tanzania, TATOA, Zakaria Hans Pope, amesema kwamba mara kadhaa serikali imeshindwa kutambua na
kusikiliza vilio vyao, hasa mpango mpya wa kukamata magari yatakayoegeshwa
barabarani.
Akizungumza mapema leo asubuhi
na kituo cha radio cha Capital Radio, Hans Pope alisema mpango huo hauna lengo
jema kwao.
Malori yakiwa yamepaki.
“Tumeweza kuzungumza mara kwa
mara na viongozi wa serikali lakini hakuna kinachosikilizwa ingawa katika vikao
hivyo tunafikia muafaka na kudai watarekebisha.
“Yapo mambo mengi ambayo kwa
kawaida yanachochea mazingira magumu ya utendaji kazi wa magari ya kubeba
mizigo na kuna kila sababu ya kuliangalia suala hili kwa ajili ya kuondoa
utata,” alisema.
Mvutano mkali umeibuka kwa siku
mbili hizi kutokana na madereva wa malori kuanza kuweka mgomo hali
inayosababisha pia mwingiliano mkubwa katika barabara hapa nchini, hususan
katika mizani.
No comments:
Post a Comment