Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za
kulipwa hapa nchini, Japhet Kaseba, amewataka vijana kuzidi kuchangamkia fursa
za mchezo huo kwa ajili ya kuonyesha vipaji vyao, sambamba na kukuza mchezo wa
ngumi.
Japhet Kaseba, pichani.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema endapo vijana watazidi kujiingiza
katika ngumi, harakati njema za kuuendeleza mchezo wa masumbwi zitashika kasi.
Alisema
anaamini huo ndio mpango wenye mashiko katika ngumi, ukizingatia kuwa bila
vijana makini na wenye uchu wa mafanikio, mambo yatakuwa magumu katika
kushuhudia mafanikio ya ngumi.
“Kikubwa
ni kuhakikisha kuwa vijana wanapata hamu zaidi ya kushiriki katika mchezo wa
masumbwi kwa ajili ya kufanikisha ndoto zao sambamba na kuongeza ushindani kwa
mabondia wote.
“Vijana
wanapoingia katika masumbwi, kila bondia anapata mshindani wake, ukizingatia
kuwa wale wanaofahamika hawawezi kubaki milele, hivyo lazima damu change
zishike kasi,” alisema.
Kaseba ni
miongoni mwa mabondia wenye mafanikio, huku akiwahi kuwa Bingwa wa Dunia wa
Ngumi za mateke, ambapo mara kadhaa amekuwa akikosa mpinzani wa kupambana naye
ulingoni.
No comments:
Post a Comment