Pages

Pages

Monday, September 30, 2013

Miss Utalii kuitangaza Dunia uhondo wa upatikanaji wa nyati hifadhi ya Ngorongoro

NYATI MWEUPE NGORONGORO MISS TOURISM TZZ
Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial Guinea Octoba 12, 2013.

Kupatikana kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu nyingine yoyote Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya Dunia, imekuwa ni fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwake , kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la Dunia Barani Afrika. 

Ambapo sasa Ngorongoro Crater  pamoja na maajabu ya bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa ajabu unao hama kila mwaka kwa umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai, lakini pia ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama katika hifadhi hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa (BIG FIVE) na adimu duniani wakiwemo Faru Weusi, Duma, Mbwa Mwitu, Kaka kuona n.k.

Ofisi ya TTB Kanda Ziwa yazinduliwa kwa mbwembwe na Naibu Waziri Nyalandu

Photo 1
Ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kanda ya ziwa iliyoko katika jingo la hotel ya Mwanza muda mfupi kabla ya kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (MB).
Photo 2
Kikundi changoma kutoka kituo cha utamaduni cha Bujora mkoani Mwanza kikitoa Burudani ya ngoma ya kucheza na chatu mbele ya ofisi ya Bodi ya Utalii kanda ya ziwa jijini Mwanza mara ru baadaya mgeni rasmi Naibu Waziri Lazaro Nyalandu kuwasili ofisini hapo ili kuizindua ofisi hiyo.
Photo 3
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazro Nyalandu (MB) akizungumza na wandishi wa habari ndani ya ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania – TTB kanda ya ziwa jijini Mwanza muda mfupi baadaya kuizindua . Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr. Aloyce Nzuki.
……………………………………………………….
 Na Geofrey Tengeneza, Mwanza
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (MB) ameiambia  ya Bodi ya Utalii Tanzania – TTB kuwa tatizo la sugu bajeti isiyotosheleza mahitaji ya Bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yake litapatiwa ufumbuzi kwa kiasi kikubwa mara baada ya fedha kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya Utalii (Tourism Development Levy kuanza) kuanza rasmi ambapo moja ya vyanzo vyake vya  fedha  ni tozo la kitanda siku kwa watalii watakaokuwa wakilala katika hoteli mbalimbali.
 
Mheshimiwa Nyalandu ameyasema hayo wakati akizindua ofisi ya Bodi ya Utalii kanda ya ziwa iliyoko jijini Mwanza. 

Amesema Bodi ya Utalii inapaswa kutengewa bajeti ya kutosha kuiwezesha kumudu ushindani uliopo wa kutangaza vivutio vyetu katika masoko ya watalii na kuvutia watalii wengi. 

Sunday, September 29, 2013

Hapa ndio stend ya mabasi ya Handeni Mjini



Hapa ndio kituo cha mabasi cha Handeni Mjini kama kilivyopigwa picha hii juzi wilayani humo mkoani Tanga. Ni tofauti na kituo cha mabasi cha Korogwe Mjini, Handeni hali inaonekana kuwa tulivu na hakuna mkanyagano sana. Hii ni kwasababu Mabasi mengi yanayopitia hapo yakitoka Tanga, Dodoma, Dar es Salaam hivyo kukusanya watu wengi mno. Picha na Kambi Mbwana.

CCM Handeni wajipanga kuvunja ngome zote za Chadema wilayani humo



Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Handeni mkoani Tanga, Athumani Malunda amesema kwamba wataendelea kujipanga ili wavunje ngome zote zinazotumiwa na vyama vya upinzani hasa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, Athumani Malunda.
Malunda aliyasema hayo siku chache baada ya kufanikiwa kuvunja ngome za Chadema katika vijiji kadhaa kikiwamo Kwamatuku ambapo zaidi ya wanachama 380 walirudi CCM.

Akizungumza wilayani hapa juzi, Malunda alisema kuvunja kwa ngome za Chadema ni hatua ya kukiimalisha chama chao Handeni na Tanzania kwa ujumla.

Alisema japo CCM haina wasiwasi na Handeni kutokana na kuheshimika kwa kiasi kikubwa, ila bado wanashawishika kuondoa dosari mbaya za kuzaliwa kwa upinzani wilayani humo.

Serikali yabariki tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga


Na Mwandishi Wetu, Handeni

SERIKALI kwa kupitia Mkurugenzi Mtendaji wilayani Handeni, mkoani Tanga, Dr Khalfany Haule, imebariki kufanyika kwa tamasha la utamaduni la Handeni Kwetu 2013, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Handeni, Dr Khalfany Haule, pichani.

Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo likiwa na lengo la kukuza na kutangaza utamaduni na utalii wa Tanzania, ukiwa ni mpango wenye mashiko kwa sekta hiyo.


Akizungumza juzi mjini hapa, Dr Haule alisema ni kitendo kinachopaswa kuungwa mkono na serikali yote ili kuongeza kasi ya kuleta maendeleo kwa kupitia njia mbalimbali.

Alisema wao kama wilaya wamepokea kwa mikono miwili wazo zuri la kuandaliwa kwa tamasha hilo wilayani Handeni mkoani Tanga, hivyo watakuwa pamoja na waandaaji.

Saturday, September 28, 2013

Kiongozi bora anatokana na maandalizi bora ya kielimu anayopata tangu akiwa shule ya Msingi



Baadhi ya wanafunzi wa darasa la pili shule ya Msingi Komsala, iliyopo wilayani Handeni, mkoani Tanga wakiwa darasani kwao kama walivyokutwa na Mpiga Picha Wetu. Wanafunzi hawa wakiendelezwa vizuri wanaweza kulipeleka mbele gurudumu la Tanzania.

Serikali yafungia magazeti pendwa ya Mtanzania na Mwananchi


Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.


Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwe na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.

Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam. Jambo ambalo halikuwa la ukweli.

January Makamba aongoza mamia ya semina ya Kamata Fursa jijini Mwanza leo

 
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Gold Crest.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest,Bwa.Mathias Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini,aliyajipatia fursa mbalimbali na kuzitumia ipasavyo na kufikia hapo alipo kimafanikio.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake,ambapo pia amewataka vijana kuitumia fursa ya ufugaji wa aina yoyote katika suala zima la kujiletea maendeleo kwa namna moja ama nyingine badala ya kusubiri Serikali iwafanyie ama iwaletee kila kitu hapo walipo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh Januari Makamba akizungumza kwenye mada yake iliyohusu masuala mbalimbali, kuhusiana na Fursa ya kuongeza thamani na kutengeneza jina, sambamba na fursa ya matumizi ya Teknolojia mbele ya maelfu ya vijana waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzzetu, iliyofanyika leo, ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza.

SIWEZI KUVUMILIA: Yanga ijiandae kushindwa na kushinda



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIKA mchezo wa soka, suala la kushinda, kutoka sare na kushindwa ni jambo la kawaida, hivyo klabu za soka Tanzania, ikiwamo Yanga, Simba lazima zijiandae kwa matokeo hayo.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, pichani.
Si ajabu timu kufungwa au kushinda. Lolote linaweza kutokea maana ni jambo la kawaida kwenye mchezo wa soka. Wakati nasema haya, nagundua jinsi baadhi ya timu zinaposhindwa kukubali matokeo ya kufungwa au kutoka sare ndani ya uwanja.
Huwa naumia kichwa ninapoona timu moja inashindwa kukubali matokeo ya kufungwa au kutoka sare. Siku zote wanataka washinde. Inapofungwa au kupata sare inalalamika mno.
Hili si jambo jema. Na ndio maana siwezi kuvumilia, hasa kwa kuanza kusikia malalamiko kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa soka Tanzania, hasa wale wa Yanga.

Kwanini tunaandaa tamasha la Utamaduni wilayani Handeni mwaka huu?


TAMKO LA KUFANYIKA KWA TAMASHA LA UTAMADUNI HANDENI

NDUGU ZANGU WATANZANIA
NDUGU ZANGU WANA HANDENI
NDUGU MDAU WA UTAMADUNI, MABIBI NA MABWANA
SALAAM!
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Kwa heshima kubwa kwako naomba niwasilishe ombi kwenu kwa mdau yoyote wa utamaduni na Mtanzania kwa ujumla juu ya kuandaa Tamasha la Utamaduni wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, ifikapo Desemba 14 mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Handeni, Dr Khalfany Haule, pichani.
Tamasha hilo tunakusudia kufanya katika Uwanja wa Azimio. Hata hivyo, Uwanja huu wa Azimio upo kwenye matengenezo, hivyo tunaweza kuendelea na tamasha letu kwa upande usiokuwa kwenye ukarabati.
Mbunge wa Handeni, Dr Abdallah Omari Kigoda, pichani.
Ndugu mdau na serikali kwa ujumla; kwa muda mrefu sasa kumekuwa kukifanyika matamasha ya kila aina katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. Kabla ya yote, napenda kuwapongeza waandaaji wote wanaoandaa matamasha hayo yenye kujenga jamii inayoheshimu utamaduni wao
Kambi Mbwana, mratibu wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Yapo matamasha mengi yanayofanyika katika mikoa hiyo na nisingependa kuorodhesha yote zaidi ya kuwashukuru na kutambua mchango wao katika sekta ya Utamaduni hapa Tanzania.

Kwa kuandaa matamasha hayo na kufanyika kwa mafanikio licha ya kuwa na changamoto za kiubinadamu, imesababisha kujenga usawa kwa wadau wa utamaduni na wananchi kwa ujumla.

Leo hii pamoja namambo mengine, lakini mtu anajiona yupo mtupu, pindi anapodharau utamaduni wao na kukimbilia tamaduni za watu wan je, hususan waliokuwa kweny Mataifa makubwa.

Ndugu zangu wadau wa Handeni Kwetu, wilaya ya Handeni ni kati ya zile zinazokabiriwa na changamoto nyingi mno. Wilaya hii iliyopakana na wilaya Korogwe, imekuwa kwenye joto kubwa la kupokea wageni mbalimbali, huku kila mmoja akiwa na utamaduni wake.

Katika tamaduni hizo, wapo wale wanaoeneza mambo mazuri na wale wanaoeneza sumu, yani tamaduni zisizokuwa nzuri nao pia hawakosekani katika utitiri huo.

Friday, September 27, 2013

Wengine wanasoma shule za gharama na wenzao wana choma mkaa



Mtoto ambaye hajaweza kupatikana jina lake mara moja akijishughulisha na kazi ya uchomaji matanuri ya matofali, kama alivyokutwa maeneo ya Kwachaga, wilayani Handeni mkoani Tanga. 

Mtoto kama huyu anastahili kutumia muda mwingi kusoma na sio kufanya kazi ya matanuri huku akiifanya kazi hiyo kwa kurithi kwa familia yake au sehemu nyingine ya jamii kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maisha yake ya kila siku. Picha na Kambi Mbwana.

JB sasa amshauri Lameck ajisalimishe Kanumba The Great, kampuni ya marehemu Kanumba



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKALI wa filamu hapa nchini, Jacob Stephen, maarufu kama JB, amemshauri Lameck Chalres Kanumba, anayejiita ni ndugu wa marehemu Kanumba kufanya mazungumzo na ndugu zake sanjari na kupewa nafasi katika Kampuni Kanumba The Great.
Msanii mahiri wa filamu Tanzania, JB pichani.
JB aliyasema hayo siku chache baada ya kuona Lameck naye ameonyesha nia ya kuingia katika soko la filamu na kufuata nyayo za marehemu Kanumba aliyefanikiwa kuwa na jina kubwa kabla ya kufariki Dunia na kuacha pigo kwa wapenzi wa sanaa nchini.
Lameck Charles Kanumba, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog mwishoni mwa wiki iliyopita, JB alisema si vyema Lameck akaanza kuhangika katika kampuni nyingine wakati kaka yake ameacha kampuni ya filamu.
Marehemu Steven Charled Kanumba, pichani enzi za uhai wake.
Alisema ni vyema msanii huyo akakutana na familia yake na wale walioachiwa kampuni hiyo ili ikiwezekana wafanye kazi kwa pamoja badala ya kuzunguuka kwa watu wengine.