Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
VYAMA vya Mpira wa Miguu
vya mikoa vinatakiwa kuendelea na mashindano ya Copa Coca-Cola yanayoshirikisha
watoto wenye umri chini ya miaka 15 katika ngazi ya wilaya wakati vikisubiriwa
vifaa na fedha za uendeshaji kutoka kwa mdhamini.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura
Kwa mujibu wa kalenda ya
mashindano (roadmap), mashindano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya yanatakiwa
kufanyika na kukamilika ndani ya mwezi Mei mwaka huu ili baadaye kuendelea na
hatua inayofuata.
Hivyo, Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawataka wanachama wake (vyama vya mpira wa
miguu vya mikoa) ambao wamejipanga kuendelea na mashindano wakati suala la
vifaa na fedha likiendelea kufuatiliwa kwa mdhamini wa mashindano.
Vifaa na fedha
zitapatikana wakati wowote baada ya taratibu husika kukamilika. Vifaa kwa ajili
ya mashindano hayo vimeagizwa kutoka nje ya Tanzania.
Ni matumaini yetu kuwa
tutakuwa na mashindano mazuri mwaka huu kulinganisha na msimu uliopita. Kampuni
ya Coca Cola ilianza kudhamini mashindano hayo mwaka 2007, na tangu mwaka huo
yamekuwa yakifanyika kila mwaka.
No comments:
Post a Comment