Mkufunzi maarufu sana aliyewahi
kupata mafanikio makubwa nchini Uingereza, Sir Alex Ferguson anatarajia kauchia ndani ndani ya timu hiyo kama
kocha wa klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu huu wa 2012/2013.
Ferguson alishinda mataji 13 ya
Ligi kuu ya soka England wakati wa uongozi wake wa misimu 26 katika klabu hiyo.
Klabu imetoa taarifa leo iliyomnukuu Ferguson akifafanua kuwa msimu huu wa 26
ndio utakaokuwa wake wa mwisho. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 71 amesema
ametafakari sana kuhusu uamuzi wa kustaafu kwake.
Amesema ameonelea ni muhimu
kuondoka katika klabu hiyo wakati ikiwa katika hali nzuri na anaamini ametimiza
hilo. Fergie amewapokonya Manchester City taji la Premier Legaue msimu huu na
kulirejesha katika uwanja wa Old Trafford ikiwa ni taji la 20 la klabu hiyo.
Kocha huyo ambaye sasa atasalia kama mkurugenzi mkuu na mjumbe wa klabu ya
Manchester United, amesema ana matumaini kuwa amejiuzulu kama mkufunzi wakati
klabu hiyo ikiwa katika hali nzuri kabisa.
Sir Alex Ferguson aliiongoza
Manchester United kutwaa taji la 20 la Premier League mwezi Aprili.
United hawajatoa dalili zozote
za ni nani atakayevivaa viatu vya Sir Alex Ferguson wakati kukiwa na uvumi kuwa
meneja wa Everton David Moyes huenda akaijaza nafasi hiyo ya katika uwanja wa
Old Trafford.
Kocha wa Real Madrid Jose
Mourinho, ambaye aliweka uhusiano mzuri wa utani wakati alipokuwa kocha wa
mahasimu wa United, Chelsea, pia amepigiwa upatu kupewa nafasi hiyo.
David Gill ambaye aliweka
ushirikiano wa kiwango cha juu cha mafanikio na Fregie kama Afisa Mkuu Mtendaji
ikiwa ni pamoja na ushindi wa mataji matatu katika msimu mmoja wa mwaka 1999 –
Premier League, Champions League na Kombe la FA, amepeana salamu za pongezi na
heri njema kwa kocha huyo.
Amesema imekwua heshima kubwa
na furaha yeye kufanya kazi na Alex kwa takribani miaka 16, kipindi ambacho
mataji mengi yamewekwa kabatini.
Ferguson anatarajiwa kufanyiwa
upasuaji wa mfupa wa nyonga mwishoni mwa msimu huu lakini kabla ya uvumi
kuanzishwa jana Jumanne, hakukuwa na dalili kuwa angejiuzulu.
No comments:
Post a Comment