Na mwandishi maalum, Riyadh - Saudi Arabia
Wanadiaspora na
Watanzania waishio Riyadh nchini Saudi Arabia walisherehekea na kuandhimisha
miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar siku ya ijumaa tarehe 12 Januari, 2018
katika ukumbi wa Riyadh Palace Hotel.
Sherehe hizo zilindaliwa na jumuiya ya
Watanzania 'Tanzania Walfare Society' ambapo waalikwa mbalimbali kutoka miji ya
Riyadh, Qasim na maeneo ya karibu walihudhuria. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo
alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe.
Hemedi Mgaza. Miongoni mwa
walihudhuria sherehe hizo pia walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu, wafanyakazi
wapya wa kampuni ya ufugaji ng'ombe wa Maziwa ya Al Marai na wengine kutoka
kampuni ya ufugaji kuku ya Al Watania. Kwa picha na habari zaidi angalia
kupitia you tube 'Prince eddycool'
Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Watanzania ya Riyadh, Bw. Fuad Mabruk akitoa hotuba mbele ya Watanzania na
wanadiaspora wa mji wa Riyadh huku nyuma yake walioketi kwenye meza kuu kuanzia
kulia ni Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya Dkt. Mahmoud Tuli, Balozi wa Tanzania
nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Afisa Mkuu wa Utawala wa Ubalozi Bw.
Ahmada Sufiani, Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Bw. Saeed Al Jabry na wa kwanza
kushoto ni Mweka Hazina wa Jumuiya Bw. Mohamed Saeed.
Baadhi ya Watanzania
na wanadiaspora wakisikiliza hotuba zilizokuwa zikitolewa na baadaye walipata
fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni.
No comments:
Post a Comment