Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla, katikati mwenye miwani, leo amekagua barabara zenye urefu wa kilometa 23 zilizojengwa miaka 2 iliyopita katika mitaa ya jiji la Mbeya na kubaini baadhi ya Barabara zilijengwa chini ya kiwango na zingine zi kuharibika na malori ya mizigo yenye uzito mkubwa kuliko uwezo wa barabara. Aidha Baadhi ya barabara kukosa mifereji ya kupitisha Maji na kusababisha uharibifu kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha TEKU
Kufuatia taarifa za wananchi juu ya Uwepo wa mashimo na kuanza kubomoka kwa baadhi ya barabara hizo imemlazimu Mkuu wa mkoa kufanya ziara kukagua barabara hizo na kuagiza mkandarasi SICO Ltd kurekebisha kasoro zote zilizojitokeza na kuongeza tanaka la lami kwa barabara soko la Kebwe yanakoingia magari makubwa na mkandarasi amekubali na kazi hiyo imeanza mara moja.
Pia ameagiza uongozi wa jiji kushughulikia Kero ya mifereji na kwakuwa Tamisemi wametoa fedha mkandarasi wa kujenga na kupanua mifereji ataanza kazi tarehe 1 julai mwaka huu
Anewataka madiwani wa halmashauri zote na jiji la mbeya kuwa makini na wafuatilisji wa miradi kwani inasikitisha kuwaona barabara iliyokabidhiwa miaka 2 iliyopita tena yenye thamani kubwa yavfedha bilioni 23 katika kipindi kifupi barabara zinakuwa na mashimo lakini hawakuchukua hatua zozote na wananchi wananungungunika
Hivyo amewataka viongozi na watalaam kutanguliza uzalendo na wahakikishe miradi inatekelezwa kwa viwango vya juu
No comments:
Post a Comment