Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi
inapenda kutoa shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa,
majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika
wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika
Kusini Jumapili ya wiki iliyopita na
kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja
mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na
kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200
kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu.
Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko
wengi mno.
Pamoja na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na
Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na
familia yao yote, Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya
Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji
Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe.