Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa, Bengi Issa mwenye kilemba, akizungumza kwenye kikao cha pamoja na Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega kushoto kwake kwa ajili ya kuangalia namna ya kushirikiana naye kuwasaidia na kuwawezesha wananchi wa Mkuranga.
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa Jimbo
la Mkuranga, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani, Abdallah Ulega, jana
amefanya kikao na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Taifa
(NEEC), Bengi Issa, kwa ajili ya kutafuta fursa ya kuwawezesha
wananchi wilayani humo.
Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa (NEEC), Bengi Issa, hayupo pichani.
Kikao hicho pia
kilihusisha Mkurugenzi wa Uwezeshaji, Afisa Maendeleo ya Jamii
Mkuranga, ambapo pamoja na mambo mengine, kilijadili namna ya
kusaidia vikundi vilivyosajiliwa 285, vikundi vya vicoba 109, ufugaji
wa nyuki, vikundi vya wanawake, vijana na waendesha bodaboda.
Akizungumza baada
ya kikao hicho kumalizika, Ulega aliyewahi pia kuwa Mkuu wa wilaya
Kilwa, alisema kwamba lengo ni kuona wanananchi wa Mkuranga wanapiga
hatua kutoka kwenye hali ya ukata na kufikia kiwango kizuri, sanjari
na kufanikisha maendeleo kwa wananchi wote.