Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(mbele kwenye Jukwaa) akipokea
Salaam ya heshima toka kwa Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa wa
Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya Uvalishaji vyeo kwa
Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza 22 ambao wamepandishwa cheo
hicho tangu tarehe 19 Septemba, 2013 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete. Hafla hiyo imefanyikia leo Oktoba 05, 2013 katika
Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga Jijini Dar es Salaam.Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimvisha cheo cha
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa
wa Arusha kwa sasa, Injinia Jeremiah Nkondo. Sherehe hizo za uvalishaji
vyeo zimefanyika leo katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na
Usalama pamoja na Serikali(hawapo pichani).Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akikagua Gwaride
Maalum lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza katika hafla fupi
ya Uvalishaji vyeo kwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza 22
ambao wamepandishwa cheo hicho tangu tarehe 13 Septemba, 2013. Hafla
hiyo imefanyika leo katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es
Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kupandishwa vyeo na Amri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.Picha zote na Lucas Mboje
wa Jeshi la Magereza
No comments:
Post a Comment