Na Kambi Mbwana, Bagamoyo
MUME wa mwimbaji wa muziki wa
taarabu hapa nchini, Khaidija Kopa, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magomeni,
Jafari Ally, ameszikwa jana katika makaburi yaliyopo mjini Bagamoyo.
Waombolezaji wakiwa katika msiba wa mume wa Khadija Kopa, leo mjini Bagamoyo.
Jeneza la Jafary Ally likiswaliwa mbele ya nyumba yake mjini Bagamoyo leo. Wa nne kutoka kulia ni mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Ridhiwan Kikwete, akiungana na waislamu wenzake kuuswalia mwili wa Diwani wa Kata ya Magomeni, mjini Bagamoyo.
Safari ya kuelekea makaburini ikaanza. Aliyebeba mwenye fulana ya mistari ni Yusuphed Mhandeni, Mchumi wa Kata ya Makumbusho CCM, jijini Dar es Salaam.Mazishi yake yalidhuhuriwa na watu wengi, wakiwamo viongozi wa vyama vya siuasa, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Serikali pamoja na wasanii wengi waliokwenda kumpa pole Kopa.
Khadija Kopa aliyefunikwa akifarijiwa kwa msiba wa mume wake mjini Bagamoyo.
Mchumi wa Kata ya Makumbusho (CCM), Yusuph Shaban Mhandeni, Yusuphed Mhandeni mwenye fulana ya mistari akibeba jeneza la Jafary Ally, mume wa Khadija Kopa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magomeni, Bagamoyo, katika mazishi yake yaliyofanyika leo mjini Bagamoyo.
Msiba wa Ally ulitikisa katika
viunga vya mji wa Morogoro, huku miongoni mwa viongozi wa juu waliohudhuria
akiwa ni Waziri wa Elimu naMafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa.
Akizungumza kwa machungu
makubwa, Khadija Kopa, alisema amejisikia uchungu mume wake kufariki huku akiwa
nje ya jiji la Dar es Salaam, huku akirejea akimkuta mumewe ni marehemu.
Alisema kuwa msiba wa mumewe
umempa uchungu mkubwa, huku akiamini kuwa utaendelea kuwa kichwani mwake
kwasababu ya kuondokewa na mume wake aliyempenda.
“Nimeuamia sana na msiba huu wa
mume wangu,” alisema Khadija Kopa, huku akibubujikwa na machozi.
Aidha, Mwenyekiti wa Baraza la
Madiwani Halmashauri ya Bagamoyo, Shukuru Mbato, alitumia muda mwingi kuwata
Watanzania wakiwamo wakazi wa Bagamoyo kuishi kwa upendo sambamba na kumuombea
marahemu aishi kwa amani katika maisha yake mapya.
“Sisi tulimpenda sana, ila
Mungu ndio muweza wa yote, hivyo sisi kama binadamu lazima tukubali matokeo,”
alisema Mbato.
Watu kutoka sehemu mbalimbali, wakiwamo wa
jiji la Dar es Salaam walijitokeza kwa wingi katika mazishi ya Ally, ambaye pia
ni mume wa Khadija Kopa.
No comments:
Post a Comment