Waziri Sonyo, mwimbaji mpya wa Victoria Sound
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI
mahiri wa muziki wa dansi hapa nchini, Waziri Sonyo, amesema nyimbo nyingi
zimekuwa nyepesi, jambo linaloweza kuangamiza soko la muziki huo nchini.
Sonyo
aliyasema hayo mapema leo, ikiwa ni siku moja baada ya kutangaza kujiunga na
bendi ya Victoria Sound, iliyokuwa chini ya Mwinjuma Muumini.
Akizungumzia
hilo, mwimbaji huyo mwenye mwili mkubwa alisema kwamba nyimbo nyingi zimekuwa
nyepesi na zinasababisha za zamani ziendelee kupendwa kuliko zao.
“Angalia
nyimbo zao za leo utashangaa kwanini waimbaji na watunzi wamekuwa wakishindwa
kuwaza na kupanga namna ya kutunga kazi bora.
“Nadhani
hili litasababisha nyimbo kuwa mbaya na wadau hawawezi kuingiza mawazo yao moja
kwa moja zaidi ya kuangalia kwenye Bongo Fleva,” alisema Sonyo.
Sonyo
anayasema hayo, huku akiwa na changamoto kubwa ya kurudisha hadhi na heshima yake
baada ya kupotea katika tasnia hiyo ya muziki wa dansi hapa nchini kwa miaka
kadhaa.
No comments:
Post a Comment