Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kimya cha muda
mrefu, hatimaye kampuni ya Push Media Mobile Limited imekabidhi zawadi za
pikipiki 14 zenye thamani ya sh. Milioni 20 kwa washindi wa mwaka huu wa
tamasha la Serengeti Fiesta.
Kampuni hiyo ilishindwa
kukabidhi zawadi hizo awali kutokana na sababu kuu moja ambayo ni malipo ya
ushuru (kodi) za kuingiza pikipiki hizo hizo nchini na kufanya zoezi hilo
kuchelewa.
Meneja Mauzo na Masoko
wa Push Mobile, Rodney Rugambo alisema kuwa kampuni yao imekabidhi pikipiki
mpya kwa washindi hao ambao wanatoka mikoa mbalimbali ambayo taamsha la fiesta
lilifanyika.
Washindi
hao ni Irene Stevens na WilliamMgala wote kutoka Dar es Salaam, Rashid Juma
Ramadhani (Tanga), Nasiru Habibu, Michael Swai (Mara), Veronica Mandisi,
Mchungaji Amos Kurubone wa Shinyanga.
Rugambo
aliwataja washindi wengine kuwa ni Mwanahamisi Msangi (Tabora), Thadey Kiwale
(Singida), Joseph Nashon Magambo, Reinatus Waitura (Morogoro) na Ali Muhamed
Sanga na Christopher Mtibwa wa Iringa.
Alisema kuwa kukabidhi
zawadi kwa washindi hao kunafanya kukamilika kwa zoezi hilo kwa mwaka huu
ambapo zawadi kubwa ya magari mawili yalikwenda kwa Diana Elisa Mkoba yenye
thamani ya shs milioni 16.
Kampuni hiyo ilitoa gari
moja moja mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza na Dodoma.
Mbali ya zawadi hizo,
kampuni hiyo pia ilitoa zawadi za simu ya mkononi aina ya Nokia dabodabo 130,
simu aina ya blackberry 14 na washindi wa fedha taslim shs milioni 20. Thamani
ya zawadi zote ni milioni 200.
No comments:
Post a Comment