https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, December 14, 2012

Handeni wajipanga kwa shida ya maji



Katibu wa Mbunge wa Handeni, Salumu Masokola pichani
Na Rahimu Kambi, Handeni
KATIBU wa Mbunge wa Handeni, Salumu Masokola, amesema kwamba mkakati uliopo sasa ni kuhakikisha kuwa wanaweka mipango madhubuti ya kuwapatia maji wakazi na wananchi wa Handeni.

Masokola ambaye ni Katibu wa Abdallah Kigoda, mbunge wa Handeni, alisema mikakati hiyo itakwenda sambamba na kupatikana visima 500 vitakavyochimbwa katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo.

Akizungumza na Handeni Kwetu mjini hapa, Masokola alisema kwamba visima hivyo vitachimbwa, ikiwa ni mikakati ya kukabiriana na shida ya maji inayoendelea kuwasumbua wakazi na wananchi wa Handeni.

Alisema mbunge wao anajua kuwa Handeni kuna matatizo ya maji kutokana na kutokuwa na vyanzo vya maji vya uhakika, lakini kwa bidii yake amekuwa akihangaikia suala hilo kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wa Handeni.

“Handeni ina kero kubwa ya maji kwasababu hakuna vyanzo vya maji vya uhakika, ila kuna mpango wa kuchimba visima 500 vitakavyogawanywa kwa kwa watu wa eneo la Handeni, hivyo kupunguza kama sio kuimaliza kabisa shida ya maji.

“Tunaamini mpango huo ukifanikiwa, wananchi wa Handeni wataishi maisha yenye amani, ukizingatia kwamba kwa sasa wimbo umekuwa ni shida ya maji na watu wanahangaika sana, hasa baada ya maji kupatikana kwa tabu,” alisema.

Kwa mujibu wa Masokola, endapo visima hivyo vitachimbwa haraka iwezekanavyo, vitagawanywa katika maeneo ya Handeni pamoja na vijiji vyake, ukiwa ni mpango utakaoleta amani kwa wakazi na wananchi wa Handeni.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...