Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
REPA wa zamani wa bendi ya Akudo Impact, Totoo ze Bingwa,
mwishoni mwa waki alifanya vitu adimu katika shoo ya bendi ya FM Academia,
maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, alipowatembelea wanamuziki na mashabiki wao
katika Ukumbi wa New Msasani Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Totoo ze Bingwa aliacha kazi Akudo Impact na kufanya kazi
kivyake, juzi alipanda jukwaa la Wazee wa Ngwasuma na kufanya makubwa,
akikumbukia ukamuaji wake wa zamani, zikiwapo rapu zake zinazotikisa katika
kona ya muziki wa dansi.
Repa huyo aliingia ukumbini hapo akiwa kama shabiki wa
muziki wa dansi, hadi pale alipooshikwa na mzuka na kuamua kujipeleka jukwaani
kwa ajili ya kuwaimbia mashabiki wa bendi ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa
Ngwasuma.
Hata hivyo huo ni utaratibu mgumu kwa Ngwasuma kufanywa,
maana mara kadhaa wamekuwa wakiwawekea ngumu wasanii kupanda jukwaani kwa ajili
ya kulinda heshima ya shoo yao
inayoingiza mashabiki lukuki katika kumbi zao.
Shoo ya juzi katika ukumbi huo ni mwendelezo wa matukio ya
kiburudani yanayofanywa na wanamuziki wakali wa bendi hiyo, wakiongozwa na Rais
wa Vijana, Nyosh El Sadaat, akiwa sambamba na Patchou Mwamba.
Nyimbo ambazo zimekuwa zikipendwa na wadau na mashabiki wao
ni pamoja na Otilia, Vuta Nikuvute, Anna na nyingine zinazowapa raha
wahudhuriaji wa shoo zao.
Akizungumzia shoo hiyo, Nyosh alisema kwamba bendi yao ipo imara na malengo
ya kufanya vyema katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.
“Tupo imara na mipango ya kuendelea kufanya makubwa katika
kona ya muziki wa dansi nchini, hivyo mashabiki wetu watuunge mkono kwa namna
moja ama nyingine, ukizingatia kwamba tuna wanamuziki wazuri na wajuzi wa
kweli,” alisema Nyosh.
Ngwasuma ni miongoni mwa bendi zenye wapenzi wengi hapa
nchini kutokana na uimara wake katika uimbaji na utunzi kutoka kwa wanamuziki
wenye uwezo wa hali ya juu, akiwamo Nyosh na wengineo wanaounda FM Academia.
No comments:
Post a Comment