Na Kambi Mbwana
VITU viliyoibwa vya marehemu Hussein Mkiety, maarufu kama 'Sharomillionea', vimesalimishwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wezi, waliompora
mara baada ya kupata ajali na kupotea uhai wake, katika kijiji cha Songa Kibaoni, wilayani
Muheza, mkoani Tanga, mapema wiki hii.
Ajali hiyo ilitokea Jumatatu saa mbili na
nusu usiku na kusababisha kifo cha msanii huyo mahiri wa uchekeshaji hapa nchini.
Msanii huyo alitokuwa
akitokea jijini Dar es Salaam
na kuelekea Lusanga wilayani Muheza kwa ajili wa kuwasalimia wazazi wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Tanga, Constatine Massawe, alithibitisha kupatikana vitu hivyo ambapo alisema
upatikanaji wake ulitokana na msako mkali uliofanya na uongozi wa
serikali wilayani Muheza wakishirikiana na Jeshi la Polisi.
Massawe alisema baada ya
kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Tanga liliweka mtego na kutangaza
kuinunua simu ya mkononi ya msanii huyo aina ya blackberry na ndipo moja kati
ya wezi ambao walihusika kwenye tukio hilo walipojitokeza na kuipeleka kwa
ajili ya kuiuza na wakati walipofika eneo ambalo walikubaliana walikabidhi simu
kwa ajili ya kuikagua na baade wezi hao kushtukia mtego huo na kukimbia huku
wakiiacha simu hiyo.
Aidha kamanda Massawe
alivitaja vitu ambavyo vimesalimishwa kwa jeshi hilo
ni simu ya mkononi aina ya Black Berry, Betrii ya gari, tairi ya akiba, radio
ya gari, begi ambalo lilikuwa na nguo za marehemu, saa ya mkononi na nguo
ambazo alikuwa amevuliwa sharomilionea na vibaka wa eneo hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo.
Kamanda Massawe alisema mpaka
hivi sasa hakuna mtu yoyote anashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia kutokea
kwa uporaji huo huku Jeshi hilo likiendelea na uchunguzi ili kuwabaini waporaji
hao na kuweza kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuweza kujibu tuhumu
zinazowakabili na kutoa wito kwa wananchi kuacha kufanya vitendo vya uporaji
pindi ajali zinapotokea katika maeneo yao.
"Tupo kwenye uchunguzi
mkali ili kuhakikisha tuwatia mbaroni wale wote ambao waliohusika na kitendo
cha kinyama alichofanyiwa msanii huyo alisema "Kamanda Massawe.
No comments:
Post a Comment