Na Kambi Mbwana, Muheza
MWIMBAJI wa muziki wa Bongo Fleva, Tunda Man, katika muda
wote wa msiba wa Hussein Mkiety, maaruru kama
Sharomillionea, alikuwa amenywea, wakati wote akiwa kimya, hivyo kuonyesha
alikuwa kwenye mawazo makubwa.
Kuanzia katika Hospitali ya Teule Muheza ulipokuwapo mwili
wa msanii Sharomillionea, Tunda Man anayetokea katika kundi la Tip Top
Connection hakuweza kusema lolote, zaidi ya kupepesa macho yake kwa majonzi.
Baada ya kumaliza taratibu za mazishi ya Sharomillionea,
msanii huyo aliyekuwa kwenye uswahiba na marehemu, alisema kuwa hakujisikia
vizuri kwa kushuhudia msanii mwenzake amelazwa chumba cha maiti na baadaye
kaburini.
“Ni mbaya sana kuangalia
kuona mtu uliyechat naye muda uliopita, au ulikuwa naye wakati Fulani
anaingizwa kaburini na kubadilishwa jina lake kirahisi
namna hii.
“Nimeumia sana kwa msiba wa
Sharomillionea, lakini sisi binadamu ni watu wa kupita hapa duniani zaidi ya
kuombeana kwa Mungu maana huwezi jua nani anafuata nyayo baada ya leo kutoka
hapa nyumbani kwa Sharomillionea,” alisema Tunda Man.
Tunda Man anatokea katika kundi la Tip Top Connection lenye
mjumuiko wa wasanii mahiri, akiwamo kiongozi wao Ahmad Ally ‘Madee’, anayejiita
pia Rais wa Manzese.
No comments:
Post a Comment