Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde, kulia akiwa na mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mjini Dodoma. Waziri Mavunde amepongeza mshindi huyo na kumtaka azitumie fedha zake kwa uangalifu ili afanikiwe kiuchumi.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mheshimiwa Anthony
Mavunde, amewataka Watanzania hususan wakazi na wananchi wa Dodoma kunufaika
kiuchumi kwa kuutumia vyema uwapo wa mchezo wa bahati nasibu wa Biko ‘Ijue
Nguvu ya Buku’.
Mh Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa makabidhiano ya Sh
Milioni 20 kutoka kwa mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, ambaye ni
fundi cherehani mwenye maskani yake mjini Dodoma, akitangazwa mshindi katika
droo ya 17.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde kulia akiwa na wananchi wake wa Dodoma Mjini walioshinda Sh Milioni 20 za Biko kila mmoja. Evodi Mlingi katikati amekabidhiwa fedha zake jana wakati kushoto ni Ramadhan Juma Hussein aliyeshinda Milioni 20 hivi karibuni ambapo tayari ameshapokea fedha zake kutoka Biko.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa kwenye tukio la kumkabidhi fedha zake mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, kushoto, mjini Dodoma jana.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri Mavunde alisema
kwamba serikali ya awamu ya Tano ni ya viwanda, hivyo ni jukumu la washindi hao
kuhakikisha kwamba wanaanzisha na kusimamia biashara kubwa kwa kutumia
mamilioni ya Biko.
Alisema fedha za Biko zinaweza kutumiwa vizuri na washindi
wao, huku katika jimbo lake, mbali na watu kuibuka na ushindi wa papo kwa hapo
unaonzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja
zinazolipwa kwa kupitia simu za mikononi za kampuni za Tigo Pesa, M-Pesa na
Airtel Money ambapo namba ya kampuni ya Biko 505050 na ile ya kumbukumbu ni
2456.
“Nawataka kila mtu ahakikishe kwamba akipata fedha hizi
anazitumia vizuri na mimi kama mbunge wao wa Dodoma nitasimamia katika
kuwapatia mwangaza mzuri wakati wowote wakihitaji, maana lengo la serikali ni
kupiga hatua kiuchumi,” Alisema.
Naye Evodi Mlingi aliwapongeza Biko kwa kuhakikisha kwamba
wamemfikishia fedha zake haraka tofauti na matarajio yake, licha ya kuwa na
imani kubwa na waendeshaji wa mchezo wa Biko ambao umekuwa ukitoa fedha nyingi
kwa washindi wao.
“Nimekuwa mchezaji mzuri wa Biko kila siku na kila saa
ambapo ninapopokea fedha ya ushindi wa papo kwa hapo naipeleka tena Biko jambo
ambalo nimepata ushindi mnono kwa kuchanganya na maombi yangu kwa Mungu, maana
nina uhitaji mkubwa wa fedha na hizi nilizopata naahidi kuzipeleka kwenye fungu
la kumi kama nilivyotaka tangu mwanzo,” Alisema Mlingi huku akiwashauri
Watanzania kucheza kwa wingi ili wapate ushindi.
Wakati huo huo, Mshindi wa droo ya 18 ya Biko ametangazwa
jana, huku akiwa ni binti mwenye miaka 25 anayeishi jijini Mbeya, Linda Mhewa,
ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu Teofilo Kisanji University (TEKU), kilichopo jijini
Mbeya.
Mwanafunzi huyo amepatikana katika droo iliyofanyika jana na
kuchezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, ikiwa ni mwendelezo
wakutoka mamilioni kwa washindi wao.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema ni
wakati wa kutajirika kwa kuhakikisha kwamba kila anayeibuka na ushindi wa Sh
Milioni 20 za Biko anazitumia katika kuanzisha au kuendeleza miradi ya
maendeleo kwa kupitia bahati nasibu ya Biko.
“Watu watumie vizuri uwapo wa Biko kwa kuhakikisha wanacheza
mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza kuanzia Sh
1,000 na kuendelea huku Sh 1,000 ikitoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa
hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambapo droo
kubwa hufanyika Jumatano na Jumapili,” Alisema.
Huku mamilioni ya fedha yakiendelea kwenda kwa Watanzania,
Biko wameshalipa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa mwezi Mei pekee, ikiwa ni zawadi
za papo kwa hapo na ile ya droo kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili.
No comments:
Post a Comment