Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DONGE nono la Sh Milioni 20 la bahati nasibu ya Biko ‘Ijue
Nguvu ya Buku’, droo ya 16, leo limeenda kwa mshindi wao Ramadhan Juma Hussein,
mwenye maskani yake mjini Dodoma, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Makao Makuu ya
Nchi ya Tanzania kupata mshindi wake katika droo kubwa inayofanyika Jumatano na
Jumapili.
Ushindi wa Ramadhan umekuja siku chache baada ya kukabidhiwa
fedha zake mshindi wa Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis, aliyekabidhiwa
pesa mapema wiki hii.
Akizungumza katika droo hiyo leo mchana, Balozi wa Biko, Kajala Masanja
alimpongeza Ramadhan kwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20, huku
akiwataka Watanzania wote kucheza kwa wingi na mara nyingi ili wazoe mamilioni
ya Biko.
“Naomba kutangaza kwamba mshindi wetu wa Jumatano hii wa Sh
Milioni 20 ni Ramadhan anayetokea mjini Dodoma, ambaye pia amekiri kucheza Biko
mara kwa mara pamoja kuwahi kushinda zawadi za papo kwa hapo ambao zinatoka
kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja
zinatoka kila dakika kwa wale wanaocheza bahati nasibu yetu.
Mchezo huu unachezwa kwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi
kwenye mitandao ya simu ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel, ambao huingiza namba ya
kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456, baada ya kufanya muamala
kuanzia Sh 1,000 na kuendelea na kupata nafasi ya kuwania zawadi za papo kwa
hapo bila kusahau kuingia kwenye droo kubwa ya Sh Milioni 20,” Alisema Kajala.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema Biko
imezidi kukolea baada ya kumpata mshindi wa Dodoma kwa mara ya kwanza tangu
waanze kuchezesha bahati nasibu yao, huku akiwapongeza wote waliowahi kushinda
donge nono la Biko kutoka kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania.
“Ni furaha kubwa kuona Dodoma wameibuka na donge nono la
Biko, huku nikiamini kuwa kucheza Biko ni rahisi pamoja na kuweza kuibuka na
ushindi wa zawadi za papo hapo bila kusahau zawadi kubwa ya Sh Milioni 20
inayotoka mara mbili kwa wiki,” Alisema Heaven.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Emmanuel Ndaki, aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za uwapo wa
bahati nasibu ya Biko, akisema kwamba ni rahisi kucheza pamoja na urahisi pia
wa kuibuka na ushindi.
“Uwapo wa mwakilishi wa Bodi kwenye droo ya Biko unatokana na
dhamira ya kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa, hivyo niwatoe hofu
Watanzania kuwa Biko ni mchezo halali unaofuata sheria zote za nchi,” Alisema
Ndaki.
Mara baada ya kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika
jana, jijini Dar es Salaam, Biko itamkabidhi mshindi wao huyo wa Dodoma jumla
ya Sh Milioni 20 kwa ajili ya kuziingiza kwenye majukumu yake ya kimaisha, huku
dalili za kupanua biashara zake kuwa kubwa baada ya kutangaza kwamba ni
mjasiriamali wa simu mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment