Jumatano hii mwingine kuzoa Milioni 20 kwa droo ya 12, cheza sasa ushinde
Balozi
wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kulia akionyesha namba ya ushindi wa
Sh Milioni ya mshindi wao wa Lupela, Makete,mkoani Njombe, Junior Ashery
Pesambili aliyepatikana katika droo ya jana Jumapili. Kushoto ni
mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
DAU nono la
Sh Milioni 10 linalotolewa kama zawadi ya droo kubwa ya Mchezo wa Kubahatisha
wa Biko limeenda kwa Junior Ashery Pesambili wa Lupela, Makete, mkoani Njombe,
ikiwa ni mwendelezo wa kugawa fedha kwa washindi wake ikitokana na matokeo ya droo
ya 11 iliyochezeshwa jana Jumapili.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akifurahia namba ya mshindi wa Sh Milioni 10 kutoka Makete, mkoani Njombe, droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam.
Droo hiyo
iliyochezeshwa jana iliendeshwa na Balozi wa Biko Kajala Masanja, akishirikiana
na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid. Akizungumza
katika droo hiyo jana, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage,
alisema wamedhamiria kugawa mamilioni kwa washindi wao wanaocheza mchezo wa
Biko uliozidi kushika kasi katika kona mbalimbali nchini Tanzania.
Alisema tayari wameshafanya droo 11 kubwa ambapo watu mbalimbali wameendelea kupokea fedha zao ikihusisha vijana bila kusahau mzee Stanley Kapondo naye aliyekuwa miongoni mwa Watanzania waliovuna zawadi mbalimbali kutoka Biko.
Alisema tayari wameshafanya droo 11 kubwa ambapo watu mbalimbali wameendelea kupokea fedha zao ikihusisha vijana bila kusahau mzee Stanley Kapondo naye aliyekuwa miongoni mwa Watanzania waliovuna zawadi mbalimbali kutoka Biko.
“Kucheza
Biko mara nyingi zaidi ndio nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, hivyo ni wakati
wa Watanzania kucheza mara nyingi ili washinde, ukizingatia kuwa mbali na donge
nono la Milioni 10 linalotolewa Jumatano na Jumapili, pia mtu anaweza kushinda
zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000,
1,000,000, huku droo ya Jumatano hii ikitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wake kama
ilivyokuwa Jumatano iliyopita.
“Mchezo wetu
unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu
za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo utakapoingia kwenye kipengele cha
Lipa Bili au lipa kwa Mpesa, mshiriki wetu ataingiza namba ya kampuni 505050 na
baadaye kuweka namba ya kumbukumbu 2456, huku akianzia kucheza kwa Sh 1000 au
zaidi,” Alisema Grace.
Naye
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, aliwapongeza
Biko kwa kuchezesha bahati nasibu inayovutia na inayotoa ushindi mnono kwa
kupitia simu za mikononi. “Ni
utaratibu mzuri unaofanywa na Biko katika kuchezesha bahati nasibu yao, hivyo
sisi watu wa Bodi tunachofanya ni kuangalia kama taratibu na sheria zinafuatwa ili
kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda vizuri, hivyo natoa rai kwa kila
Mtanzania kucheza Biko ili waibuke na ushindi,” Alisema Maggid.
Akizungumza
kwa simu wakati anatangazwa, mshindi huyo hakusita kuonyesha furaha yake,
akisema haamini kama ameshinda Milioni 10 za Biko akiongeza kwamba ni wakati
wake kukuza uchumi wake kwa kupitia mchezo wa Biko ambao umekuja na kuboresha kipato chake.
“Nashukuru kutangazwa
mshindi wa droo ya 11 ya Biko, ambapo kushinda kwangu naamini ni wakati muafaka
sasa wa kufanikiwa kimaisha kwa sababu Mungu amepanga jambo zuri kwangu,ukizingatia
kwa sasa najishughulisha na kazi ya uchanaji wa mbao” Alisema. Baada ya
kuibuka na donge hilo, mshindi huyo wa Biko anatarajiwa kukabidhiwa fedha zake
haraka iwezekanavyo ili aziingize kwenye matumizi yake ya kimaisha kwa ajili ya
kuinua kipato chake.
No comments:
Post a Comment