Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya 12 ya Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’
imechezeshwa leo asubuhi, huku ikimpata mshindi wake wa nonge nono la Sh Milioni
20 ikiwa ni maalum kwa Jumatano hiyo kutoa mshindi wa Sh Milioni 20 ambapo
mkazi wa Arusha, Oscar Haule kuibuka kidedea kwa kuzoa mamilioni hayo.
Donge nono hilo limekwenda kwa mshindi huyo wa Arusha, ikiwa
ni mwendelezo wa kutoa mamilioni katika zawadi mbalimbali za bahati nasibu huyo
inayoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni
moja kwa zawadi za hapo hapo huku droo kubwa ya Jumatano na Jumapili hii pia
itatoa Sh Milioni 20 kama Jumatano mbili zilizopita.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akichezesha droo ya 12
ya Bahati Nasibu ya Biko, ambapo mkazi wa Arusha, Oscar Haule alitangazwa
mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.
Akizungumza leo asubuhi katika uchezeshaji wa droo hiyo, Meneja Masoko
wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba ni wakati wa kushinda mamilioni ya
Biko kwa kuchezesha bahati nasibu yao rahisi na yenye nafasi kubwa ya ushindi
wa zawadi za papo kwa hapo na zile za wiki zinazotoa mamilioni kwa droo ya
Jumatano na Jumapili.
Alisema hadi sasa zaidi ya washindi 55,000 wameshinda zawadi
kutoka Biko, huku wakiamini kuwa Biko ni chanzo cha mapato na kinachoweza
kubadilisha maisha ya washindi wao wanaoamua kujitokeza kwa wingi kuwania
mamilioni kwa kupitia mchezo huo.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akichezesha droo ya 12
ya Bahati Nasibu ya Biko, ambapo mkazi wa Arusha, Oscar Haule alitangazwa
mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari Maggid kushoto akiandika namba ya ushindi ya mkazi wa Arusha, Oscar Haule katika droo ya Sh Milioni 20 iliyochezeshwa leo.
“Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu kila mtu anaweza kucheza
kwa kupitia simu yake ya mkononi hususan kwa Tigo, Vodacom na Airtel ambapo
wataingia kwenye vipengele cha kufanya miamala kwenye simu hizo kwa kuingiza
naamba ya kampuni ambayo ni 505050, huku namba yetu ya kambukumbu ikiwa ni
2456.
“Hakuna njia ya mkato ya kushinda Biko badala yake watu
wanapaswa kucheza kwa wingi na mara nyingi zaidi ili wajiwekee nafasi nzuri za
ushindi, ukizingatia kuwa ndio sababu kubwa ya ushindi maana kila anayecheza
Biko jua anaweza kubadilisha maisha yake kama atashinda zawadi za papo hapo
pamoja na ile droo kubwa ya Sh Milioni 10 hadi 20 kwa Jumatano hii na ile
iliyopita pamoja na Jumapili inayokuja ambapo bado siku chache mshindi
apatikane,” Alisema.
Akizungumza katika droo hiyo, Mwakilishi wa Bodi ya Michezo
ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid aliwapongeza washiriki wote wanaocheza
mchezo wa Biko na kuwataka waendelee kutumia vyema fursa za kuibuka na
mamilioni kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko iliyojizolea umaarufu tangu kuanzishwa kwake nchini.
“Bodi inafurahishwa na uchezeshwaji wa bahati nasibu ya
Biko, hivyo tunawataka watu wajitokeze kwa wingi kucheza Biko ili wavune zawadi
mbalimbali kutoka kwenye bahati nasibu hii ambayo ni rahisi kucheza na rahisi
pia kushinda kwake,” Alisema.
Naye Oscar Haule aliyetangazwa mshindi katika droo ya jana
ya Sh Milioni 20, aliishukuru Biko kwa kuchezesha droo hiyo iliyompa ushindi
mnono na kusema kuwa hakuamini kama angewezaa kutangazwa mshindi wa zawadi
kubwa inayotolewa Jumatano na Jumapili.
“Nashukuru sana kwa hilo maana nikipata pesa hizo
zitanisaidia kukwamua changamoto zangu za kimaisha pamoja na kupata mwangaza wa
namna gani nitajihakikishia maisha mazuri kwa kutumia pesa hizo katika shughuli
zangu za kila siku,” Alisema.
Biko ni Bahati nasibu iliyojizolea umaarufu mkubwa nchini
Tanzania huku ikitoa mamilioni kwa washindi wake wanaoshinda zawadi za droo
kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili sambamba na wale wanaopokea fedha za
ushindi wa papo kwa hapo kwa kupitia simu za walizotumia kuchezea bahati nasibu
hiyo ya aina yake.
No comments:
Post a Comment