Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MOTO wa bahati nasibu ya Biko ama ‘Ijue Nguvu ya Buku’,
umezidi kuchanja mbuga baada ya droo yake ya 14 kufanyika leo jijini Dar es
Salaam, huku mkazi wa Kilosa Morogoro, Magreth Sinyangwa, akiwa mwanamke wa
kwanza kuzoa jumla ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji wa bahati
nasibu hiyo inayotikisa hapa nchini.
Droo hiyo iliyompelekea utajiri mshindi huyo wa Morogoro,
imechezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja na kushuhudiwa pia na
mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akiagana na mwakilishi wa Bodi Michezo ya
Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein, mara baada ya kumaliza
kuchezesha droo ya 14 ya Sh Milioni 20 iliyochezeshwa leo jijini Dar es
Salaam, huku Magreth Sinyangwa akiwa mwanamke wa kwanza kuibuka na
mamilioni hayo ya Biko tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu hiyo hususan
kwa droo kubwa za Sh Milioni 10 hadi 20.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa droo hiyo, Meneja
Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema moto wa Biko umezidi kuchanja mbuga
baada ya kumpata mshindi wao wa Sh Milioni 20, huku kwa mara ya kwanza
wakimpata mshindi ambaye ni mwanamke tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu yao.
Alisema washindi hao ni wale wanaocheza bahati nasibu yao kwa
njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za
M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money, ambapo watatakiwa kuingia kwenye lipa bili
au lipa kwa M-Pesa na kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na namba ya
kumbukumbu 2456 tayari kwa kucheza.
“Baada ya kuingiza namba ya kumbukumbu pia atatakiwa kuweka
kiasi cha kucheza ambacho kinaanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo kiasi cha Sh
1000 kitampatia nafasi mbili ambazo ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na donge
nono la Sh Milioni 20 kwa Jumapili ijayo kama tulivyompata mwingine kwa droo
tuliyochezesha jana.
“Kwa zawadi za papo kwa hapo zinaanzia Sh 5000, 10,000,
20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja ambapo mshindi hutumiwa
fedha zake dakika chache baada ya kupokea ujumbe wa Biko ukimtaarifu juu ya
ushindi wake kutokana na kucheza Bahati Nasibu yetu,” Alisema Heaven na
kuwataka Watanzania wacheze mara nyingi zaidi ili waweze kujiwekea mazingira
mazuri ya kuibuka na zawadi mbalimbali za Biko.
Naye mshindi huyo Magreth Sinyangwa akizungumza kwa simu
baada ya kutangazwa mshindi wa Sh Milioni 20 alisema hakuamini kama ameshinda
kiasi hicho cha pesa baada ya kujulishwa hivyo na Kajala, huku akisema kuwa
amepokea kwa furaha kwa sababu zitamkwamua katika shughuli zake za ujasiriamali.
“Nashukuru Biko kwa kunijulisha juu ya ushindi wangu mnono wa
Sh Milioni 20 ambazo kwa hakika zimekuja wakati muafaka kwa sababu tayari
nimepata kitu cha kuniletea utajiri mkubwa kutokana na kushinda kwangu donge
nono la Biko kama waliyokuwa wanashinda wengine,” Alisema Magreth.
Naye Humud Abdulhussein ambaye ni mwakilishi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania, alisema mchezo wa Biko unafuata kanuni, sheria
na taratibu zote zilizowekwa na serikali kwa kusimamiwa vizuri na Bodi yao ili
kuhakikisha michezo ya kubahatisha inakuwa salama.
Bahati Nasibu ya Biko imekuwa ikizidi kutoa washindi wengi wa
papo kwa hapo na wale wanaoshinda zawadi kubwa ya Sh Milioni 10 hadi 20, huku
jumla ya Sh Milioni 500 zikitolewa kwa mwezi Mei pekee, jambo linaloashiria
mafanikio makubwa kwa wanaoshiriki mchezo huo wa Biko.
No comments:
Post a Comment