Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO
ya 13 ya Biko waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha Tanzania maarufu
kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’, imefanyika leo asubuhi, huku mkazi wa Mbezi jijini
Dar es Salaa, Amani Kabuku, mwenye miaka 23, akifanikiwa kuibuka na
ushindi mnono wa Sh milioni 20.
Mshindi
huyo ameibuka katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam na
Balozi wa Biko, Kajala Masanja, kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi
ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Kajala Masanja kulia akizungumza huku akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam baada ya kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, huku akishuhudiwa na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
“Wanachotakiwa
kufanya ni kucheza mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri
yaushindi wa zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000,
100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku zikilipwa moja kwa moja
kupitia simu zao za mikononi walizotumia kuchezea Biko,” Alisema Grace.
Naye
Balozi wa Biko Kajala Masanja aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi
kucheza Biko ili wajipatie chanzo kipya cha uchumi ili wajiendeshe
kiuchumi.
“Huu si muda
wa kuachia wengine wajipatie fedha huku wengine tukikaa tu, badala yake
wote tuamke ili kuchangamkia fursa ya kiuchumi kwa ajili ya kupata mtaji
kwa ajili ya kujiendesha kimaisha kwa namna moja ama nyingine,”
Alisema.
Akizungumzia
ushindi wake, mshindi huyo kutoka Mbezi, Amani aliwashukuru Biko kwa
kumtangaza mshindi utakaompatia jumla ya Sh Milioni 20 ambazo
zitamsaidia kwa kiasi kikubwa katika vitu vitakavyomuwezesha kiuchumi.
“Nashukuru
kwa kutangazwa mshindi wa Biko wa droo ya 13 ambayo kama nikipata fedha
hizo Sh Milioni 20 hakika nitazitumia vizuri katika kuinua kipato
change, ukizingatia kuwa nilicheza Biko kwa malengo ya kushinda kwa
kumuomba Mungu,” Alisema Amani.
Kwa
kutangazwa mshindi huyo, Biko wanatarajia kumpatia zawadi yake mapema
wiki hii kwa ajili ya kuhakikisha kwamba anaziweka katika matumizi yake
ya kuinua uchumi wake, huku mamilioni mengine yakiendelea kutoka kwa
ushindi wa papo kwa hapo pamoja na Sh Milioni 20 kwa droo ya Jumatano
hii.
No comments:
Post a Comment