KATIKA hali inayoonyesha ya kuchachamaa na kuchangamkia
fursa, droo ya 17 ya Bahati ya Nasibu ya Biko ‘ijue Nguvu ya Buku, imefanyika
jana jijini Dar es Salaam, huku fundi charahani wa Mjini Dododoma, Evodi
Mlingi, kuibuka kidedea na kujinyakulia jumla ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na
Biko.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza na simu ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Dodoma, Evodi Mlingi aliyepatikana baada ya kuchezesha droo ya 17 ya Bahati Nasibu ya Biko. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki.
Droo ya kumtafuta mshindi huyo wa Sh Milioni 20 imeendeshwa
na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Biko,
Goodhope Heaven, alisema Mlingi ni mshindi wa pili wa anayetokea Dodoma mjini
kujinyakulia Sh Milioni 20, akitanguliwa na Ramadhan Juma Hussein, aliyekabidhiwa
fedha zake wiki iliyopita.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, akiandika dondoo baada ya kupatikana kwa mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 17 ambapo Evodi Mlingi mkazi wa Dodoma aliibuka kidedea. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
Alisema mchezo wa Biko ni rahisi kucheza na rahisi pia
kushinda kwa kutumia simu za mikononi za kampuni za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel
Money, ambapo wanachotakiwa ni kufanya miamala kwenye simu zao kuanzia Sh 1,000
na kuendelea huku namba ya kampuni wakipaswa kuingiza 505050 na ile ya
kumbukumbu ni 2456.
“Huu ni wakati wa kutajirika kwa kupitia Biko, hivyo
tunampongeza mshindi wetu wa Dodoma, Mlingi kwa kushinda dodo la Sh Milioni 20,
huku nikiwakumbusha kuwa kila mtu anaweza kushinda zawadi mbali mbali za fedha
taslimu za papo kwa hapo kuanza Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000,
500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwenye simu za washindi,”
Alisema.
Naye mshindi huyo wa Dodoma, Mlingi aliwashukuru Biko kwa
kumtangaza mshindi katika droo ya 17, huku akisema sasa maisha yake yamekuwa
mazuri kwa kuzitumia vizuri fedha za bahati nasibu hiyo atakazopewa.
“Nilikuwa nacheza Biko kwa malengo ya kushinda, hivyo leo
kutangazwa mshindi hatimae ndoto zangu zimetimia, maana pamoja na kucheza sana,
pia nilikuwa namuomba Mungu anipe nafasi ya mimi kushinda ili niimudu familia
yangu,” Alisema kwa hisia fundi charahani huyo kutoka Dodoma Mjini.
Kwa upande wake mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, Emmanuel Ndaki, aliwapongeza Watanzania wote wanaojitokeza kwa wingi
kucheza Biko akisisitiza kuwa ni eneo zuri la kunufaika kuichumi kwa kupitia
sekta ya michezo ya kubahatisha.
“Watanzania wacheze kwa wingi kwa sababu ni mchezo unaofuata
vigezo vyote kutoka kwenye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, nikiamini kuwa
wanaweza kujikomboa kiuchumi kwa kupitia fursa ya michezo hii ya kubahatisha
hapa nchini,” Alisema.
Kwa kutangazwa mshindi kwenye droo ya 17, sasa Mlingi
anajiandaa kupokea fedha zake haraka iwezekano kutoka kwa waendeshaji wa bahati
nasibu hiyo ambao Mwezi Mei pekee waliweza kutoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa
washindi wao.
No comments:
Post a Comment