Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MFANYABIASHARA wa simu za mikononi mjini Dodoma, Ramadhan
Juma Hussein, jana amejazwa Sh milioni 20 zake alizoshinda kutoka kwa
waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko, aliyoshinda katika droo ya 16,
iliyochezeshwa Jumatano iliyopita.
Mshindi wa droo ya 16 ya Sh Milioni 20 kutoka Biko,
Ramadhan Juma Hussein katikati akiwa amebeba fedha zake alizokabidhiwa
jana na waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko mjini Dodoma katika benki
ya NMB. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Kupokea kwa pesa zake kumekuja baada ya kuwa miongoni mwa
Watanzania lukuki wanaocheza bahati nasibu ya Biko kuwania zawadi za papo kwa
hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni
1,000,000, pamoja na donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka Jumatano na
Jumapili.
Meneja
Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni
20 mshindi wao wa Dodoma, Ramadhan Juma Hussein. Wengine wanaoshuhudia
ni familia ya Ramadhan wakati wa makabidhiano hayo.Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika benki ya NMB mjini Dodoma, Juma anasema kwamba pesa hizo atazitumia vizuri katika kukuza biashara zake kama alivyokuwa akimuomba Mungu aweze kushinda mamilioni ya Biko.
Ramadhan
Juma Hussein akiwa kwenye fyraha baada ya kukabidhiwa jumla ya Sh
Milioni 20 kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko. Makabidhiano
hayo yalifanyika jana katika benki ya NMB Mjini Dodoma.
“Nashukuru nimekuwa mchezaji mzuri wa Biko na huwa nashinda
mara kwa mara zawadi za papo kwa hapo ambazo hupatikana kwa kufanya miamala
kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea
ambapo namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.
“Binafsi ninawaamini Biko kwa sababu si mara ya kwanza
kushinda zawadi za papo kwa hapo, hivyo nawaomba Watanzania wenzangu tujitokeze
kwa wingi kucheza Biko ili tushinde zawadi mbalimbali ikiwamo hii ya Milioni 20
ambayo leo nimekabidhiwa, huku nikiahidi kuwa nitaendelea kucheza Biko zaidi na
zaidi,” Alisema.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba wanaendelea
kusambaza mamilioni kutoka kwa washindi wao mbalimbali wanaojitokeza kwa wingi
kucheza bahati nasibu yetu rahisi katika uchezaji wake.
“Huu ni wakati wa kulala masikini na kumka tajiri kwa sababu
kwa kupitia Biko kila mtu anaweza kuvuna mamilioni yetu ya papo kwa hapo pamoja
na donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili,” Alisema.
Biko ni mchezo wa bahati nasibu uliojizolea umaarufu mkubwa
nchini Tanzania kwa siku chache tangu kuanzishwa kwake, huku kwa mwezi Mei
pekee zaidi ya Sh Milioni 500 zikiwa zimekwenda kwa washindi waliobuka katika
nafasi mbalimbali za ushindi.
No comments:
Post a Comment